Habari za Punde

Walio katika mazingira magumu wasaidiwa barakoa

NA Takdir Suweid

Wananchi wametakiwa kuwa Wazalendo na kuweka utaratibu wa kusaidiana wakati yanapotokea matatizo ili kuzidisha upendo na Ushirikiano baina yao. 

 Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini kichama Talib Ali Talib wakati wa zoezi la kugawa Vibarakoo huko Amani Wilaya ya Mjini. 

 Amesema baadhi ya Wananchi wanaishi katika hali ngumu hivyo wanahitaji kuungwa mkono kwa kupatiwa misaada mbalimbali. 

 Aidha amesema lengo la kutoa vibarakoa bila ya malipo ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na janga hilo linaloithakili Dunia. 

 Hata hivyo amesema Vibarakoa hivyo vinatolewa kwa Wananchi wanaohitaji bila ya Ubaguzi wa Kisiasa, Dini, Jinsia na Ukabila. Mbali na hayo amewaomba Wananchi kufuata maelekezo yanayotolewa na Wataalamu wa Afya ili kuweza kujikinga na Corona.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.