Habari za Punde

Rais Dk Shein afanya uteuzi wa viongozi wa taasisi za serikali

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-

1. Dkt. Juma Malik Akil ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Zanzibar.

2. Dkt. Suleiman Shehe Mohamed ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, Zanzibar.

3. Dkt. Hussein Khamis Shaaban ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara, Zanzibar.

4. Bibi Fauzia Sinde Hassan ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara, Zanzibar.

5. Bwana Haji Ali Zubeir ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Barabarani, Zanzibar.

6.Bwana Hussein Abdi Hassan ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Karakana Kuu ya Magari, Zanzibar.

7. Bibi Sheikha Ahmed Mohamed ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Meli na Uwakala, Zanzibar.

8. Kaptein Dkt. Hamad Bakari Hamad ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Ujenzi ya Serikali.

9. Bwana Shaabani Haji Chum ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali Mtandao, Zanzibar.

10. Bwana Salum Said Ali ameteuliwa kuwa Mrajis wa Baraza la Wataalaam wa Maabara za Afya, Zanzibar.

11. Bwana Mohamed Mwalimu Simai ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Vipimo, Zanzibar.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 17, Juni 2020.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.