Habari za Punde

Wanachama wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Wajitokeza Kumdhamini Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Mhe.Dk.John Pombe Magufuli

KATIBU wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba Ali Khamis Juma, akihakiki kadi ya mmoja wa Vijana wa UVCCM aliyejitokeza kumdhamini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, udhamini huo  umefanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi.

MMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba, akitia saini ya kumdhamini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, udhamini huo  umefanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba Yussuf Ali Juma, akiwaonyesha vijana wa Chama cha Mapinduzi wa mkoa huo, Fomu ya kumdhamini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, ujazaji wa Fomu hiyo umefanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi.
BAADHI ya Vijana wa Mkoa wa Kusini Pemba wakionyesha kadi zao za Chama cha Mapinduzi CCM, ikiwa ni ishara ya kukubali kumdhamini Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, udhamini huo umefanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.