Habari za Punde

WAZIRI WA AFYA HAMAD RASHID MOHAMED ATEMBELEA KAMBI ILIOKUWA YA AGONJWA WA CORONA ZANZIBAR.

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa jeshi la kujenga uchumi Zanzibar [JKU] wakati akikagua maeneo mbalimbali   yaliyokua yakitumika kwa ajili ya wagonjwa wa Corona.
Waziri wa Afya  Hamad Rashid Mohammed akizungumza na Maofisa wa Jeshi la kujenga uchumi mara baada  ya kuwatembelea kwa lengo la kukagua kambi iliyokua ikitumika kwa kulaza wagonjwa wa Corona,hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa skuli ya JKU iliyopo Mtoni Zanzibar 
Waziri wa Afya  Hamad Rashid Mohammed (kulia)akisisitiza jambo wakati akiwa katika moja ya chumba kilichokua kikitumika kutoa huduma kwa wagonjwa wa Corona  Skuli ya JKU Mtoni Zanzibar. 
Waziri wa Afya Hamad Rshid Mohamed akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa jeshi la kujenga uchumi Zanzibar [JKU] wakati akikagua maeneo mbalimbali   yaliyokua yakitumika kwa ajili ya wagonjwa wa Corona. 

Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid Mohammed akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa afya mara baada ya kukagua kituo cha afya cha Fujoni ambacho ni miongoni mwa  vituo vilivyoteuliwa kutoa huduma za mwanzo kwa wagonjwa wenye dalili za Corona endapo wakitokezea 

PICHA NA-FAUZIA MUSSA/MAELEZO ZANZIBAR.

Na Isaa Mzee,Maelezo 26/6/2020
Waziri wa Afya Mh.Hamad Rashid Muhamed amelipongeza Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) kwa kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kupambana na Maradhi ya corona kwa kutoa jengo lao ikiwa ni mojawapo ya kambi ilio tumika kulazwa wagonjwa wa maradhi hayo.
Pongezi hizo alizitoa huko mtoni katika skuli ya JKU wakati alipo kua akitembelea kambi hiyo mara baada ya kutokuwepo mgonjwa hata mmoja kambini hapo wa maradhi yanayo sababishwa na virusi vya corona.
 “Hivi sasa hatuna mgonjwa yoyote katika vituo vyetu, nasisitiza maradhi haya bado yapo na yanauwa  lazima tusijisahau tuendelee  kuchukua tahadhari kama kawaida,  atakae hisi dalili afike kituoni kwa huduma  ” alisema waziri
Aidha waziri huyo alishukuru kwa kusema kwa sasa wamefikia asilimia kubwa kuyatokomeza maradhi hayo hapa Zanzibar hivyo wananchi wazingatie zaidi maelekezo yanayo tolewa na wataalamu wa afya.
Hatahivyo waziri huyo aliwatoa hofu  maafisa hao na kuwahakikishia kuwa jengo hilo kwa sasa lipo salama na wanaweza kuendelea na shughuli zao za kimasomo.
Kwa upande wake mkuu wa utawala wa Jeshi la kujenga uchumi Mtoni Kanali Mussa Shaame amemshukuru waziri huyo kwa kuwatoa wasiwasi na kuahidi kumpa ushirikiano katika kupambana na janga hilo.
“sisi kama Jeshi la kujenga uchumi tunafahamu wajibu wetu kwa wananchi na Serikali ndio maana tuliamua kuipatia Serikali jengo hili ili kudhibiti maradhi haya mabaya na tunafahamu kuwa maeneo ya Jeshi hutumika kwa dharura za kiserikali hivyo tumetimiza wajibu wetu” alisema kanal Mussa.
Katika ziara hiyo Waziri huyo alipata nafasi ya kukagua  baadhi ya   vituo vya afya katika ngazi za wilaya  ambavyo vimeandaliwa kwa ajili ya kuvipa uwezo wa kutoa huduma ya mwanzo  kwa mtu mwenye dalili ya maradhi ya corona iwapo amegundulikana.
 Alifafanua  kua wizara imeamua kuweka vituo 20 katika wilaya zote Unguja na Pemba ambapo 14 Unguja na sita Pemba ili kurahisisha huduma  katika kupambana na kudhiti ugonjwa huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kinga Dk.Fadhil Mohamed Abdallah amesema lengo kuu la kuweka vituo hivyo wilayani ni kurahisisha na kupata uhakika wa taarifa za mtu mwenye dalili ili kupewa huduma ya  uhakika.
“Huu ni utaratibu mpya tumeuanzisha wilayani ili kupambana na maradhi hayo,tunawataka wahudumu wa afya wavitumie vituo hivyo kwa kuwapatia elimu wananchi  ya kujikinga na maradhi haya”.alisema mkurugenzi.
 Miongoni mwa vituo vilivyokaguliwa ni pamoja na kituo cha Afya cha Selemu Mfenesini,Fujoni na Matemwe.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR  26/6/2020




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.