Habari za Punde

Wananchi Zanzibar wahamasishwa kujitokeza kutoa damu baada ya kupungua ugonjwa wa Corona


Waziri wa Afya Hamad Rashid Muhamed akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Mnazimmoja kuhusu maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu Dunia ambayo hufanyika kila ifikapo tarehe 14 Juni ya kila mwaka na kuwataka wananchi kujitokeza kuchangia damu baada ya kupungua maradhi ya Corona.

 Meneja Kitengo cha damu salama Zanzibar Dk. Salama Rashid Abdalla akitoa neno la shukrani kwa waandishi wa habari na washiriki wa mkutano uliozungumzia maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu Duniani uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

Picha na Makame Mshenga

Meneja uhusiano Kitengo cha damu salama Zanzibar Bakari Magarawa akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano uliohusu maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu Dunia uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.