Habari za Punde

Mkutano Mkuu wa Jimbo la Mahonda wa Kura ya Maoni Kuwachagua Mbunge na Mwakilishi Kupeperusha Bendera ya CCM Katika Uchaguzi Mkuu Mwaka huu..

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM  Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Mahonda  wa  kupiga Kura za Maoni za wapeperushaji wa Bendera ya Chama cha Mapinduzi  katika nafasi za Ubunge pamoja na Uwakilishi kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba Mwaka huu hapo Ukumbi wa CCM Mkoa Mahonda.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Mahonda wakifuatilia salamu za Balozi Seif hayupo pichani kwenye Mkutano wao wa kuwapendekeza Wajumbe watakaowania fursa ya Uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Tifa akiwa pia Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la Mahonda akipiga kura yake kuwapendekeza Wanachama wa watakaochaguliwa kuwania nafasi ya Uwakilishi na Ubunge kwenye Uchaguyzi Mkuu ujao.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Mahonda  wa  kupiga Kura za Maoni kwa kuwapendekeza watakaowania nafasi za Ubunge na Uwakilishi kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi Oktoba Mwaka huu.
Picha na OMPR

Na.Othman Khamis OMPR.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema kigezo cha Uongozi bora wa kuutumikia Umma kinapimwa kutegemea umahiri wa Mtu aliyeshiba Uzalendo unaothubutu kuwa tayari kusimamia Maendeleo ya wale aliokubali kuwasimamia.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akitoa salamu kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Mahonda  wa  kupiga Kura za Maoni za wapeperushaji wa Bendera ya Chama cha Mapinduzi  katika nafasi za Ubunge pamoja na Uwakilishi kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba Mwaka huu.
Mkutano huo uliosimamiwa na Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini “B” umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja iliyopo Mahonda.
Balozi  Seif Ali Iddi akiwa Mjumbe wa Mkutano huo aliyemaliza muda wake wa Ujumbe wa Baraza la Wwakilishi wa Jimbo la Mahonda alisema Wajumbe hao wana Kazi nzito ya kumchagua Mwanachama atakayeendeleza maendeleo yaliyopatikana katika vipindi vya Miaka iliyopita.
Alisema kura za Wajumbe hao ambazo zina thamani ya kipekee kwa vile ina uwezo mkubwa wa kubainisha ni kwa kiasi gani yule waliyemteua ameshiba umahiri wa kuwasimamia vyenginevyo ni kudumaa kwa  Maendeleo ya Jimbo ndani ya kipindi cha Miaka Mitano ijayo, kitu ambacho asingependa kukishuhudia.
“ Nitafurahi sana iwapo tutawachagua Wanachama wenzetu waliyo mahiri na nguvu za Kizalendo zitakazoyaendeleza yale mazuri tuliyoyakuta na kuyaacha sisi kwa mustabali wa Umma “. Alisema Balozi Seif.
Mjumbe huyo  wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM aliwapongeza Wananchi na Wana CCM wa Jimbo la Mahonda kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chake chote cha Miaka Mitano katika kuwatumikia Wananchi wa Jimbo hilo.
Alisema kwa vile alitoa indhari ya kutoendelea na nafasi ya Uwakilishi ifikapo Mwaka huu wa 2020 takriban Mwaka Mmoja na nusu uliopita nyuma ameelezea matumaini yake kwamba Wananchi na Wanachama wametumia nafasi hiyo kutafakari kwa makini kumpata mrithi makini kitendo ambacho ana matumaini makubwa ya mrithi huyo kuendelea kuleta mageuzi makubwa ya Maendeleo ndani ya Jimbo la Mahonda linalobadilika kila kukicha kuwa na harakati za Maendeleo na Kiuchumi.
Mapema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Mahonda Ndugu Farahan  Haji Othman akiufungua Mkutano huo wa CCM Jimbo alisema Uchaguzi ni matokeo yanayopembua Watu wanaogombea au kushindania fursa za nafasi tofauti za kubeba jukumu.
Nd. Farahan alisema kwa vile mchakato huo hubeba makundi mbali mbali ya Waomba nafasi hizo ni vyema pale unapofikia wakati wa kumpata mmoja miongoni mwao kinachoendelea mbele ni makundi yote kurejea katika Umoja na Mshikamano mfumo unaojenga umoja na hatimae lengo la michakato hiyo hufikiwa kwa mafanikio makubwa.
Mchakato huo wa Kura za Maoni ndani ya Jimbo la Mahonda  umewashirikisha waomba ridhaa wapatao 15 kwa nafasi ya kugombea Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi na  15 kwa nafasi ya Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi kwa ajili ya Uchaguzi ujao wa Vyama vingi vya Siasa Nchini.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Jimbo kwa mujibu wa Kanuni na Utaratibu wa Chama cha Mapinduzi katika Kikao chao cha baadae ndio watakaopendekeza Majina Matatu ya Uwakilishi na Matatu ya Ubunge  kupelekwa Mkutano Mkuu wa Wilaya na baadae ngazi zinazofuata kwa hatua nyengine za Kichama.
Waomba ridhaa hao ni pamoja na Ali Salum Jecha, Khamis Salum Ali, Abdullah Hemed Mussa, Ussi Makame Kombo, Asha Abdullah Mussa, Salum Mbarak Moha’d, Simba Haji Mcha, Kamal Abdulsatar Haji, Ummukulthum Ambar Ujudi, Dhamir Makame Baro, Jadi Moh’d Said, Ali Moh’d Haji, Mtenge Makame Faki, Yussuf Abdullah Moh’d na Omar Ali Hassan.
Kwa upande wa Kura ya Maoni nafasi ya Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi Jimbo hilo la Mahonda  walioomba ridhaa hiyo walikuwa wabombea 15 Ambao ni pamoja na Mtumwa Rashid Khalfan,Bahat Ali Abeid, Moha’d Juma Moh’d, Ali Moh’d Choum na Hamod Salmin Amour.
Wengine ni Hilika Fadhil Khamis,  Haji Fadhil Mkadam, Mtuma Juma Mshamba, Abdulla Ali Hassan, Ali Abdullah Ali Othman Daud Suleiman, Khamis Mtumwa Ali, Makame Mshimba Mbarouk, Privatus Evar Kakamagige pamoja na Juma Said Moh’d.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.