Habari za Punde

Zantel Yazindua Huduma ya Halikati Bando Wateja Kuweza Kuvusha Dakika na Mb Zilizosalia Kwenda Kifurushi Kipya.


Mkuu wa Bidhaa na Huduma Zantel Aneth Jamilla Muga akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Ofa ya Huduma ya Bando Halikati iliofanyika katika Duka la Zantel Vuga Jijini Zanzibar. 

Ule wasi wasi wa kupoteza dakika na Mbs za intaneti pale kifurushi chako kinapoisha muda wake kwa sasa imebaki kuwa historia kwa wateja wa Zantel baada ya Kampuni hiyo kuzindua huduma maalumu ijulikanayo kama Halikati.

Huduma hiyo ya aina yake inamuwezesha mteja kuvusha dakika na MBs zilizosalia kutoka kwenye kifurushi cha awali kwenda kifurushi kipya na kumpa uwezo wa kuongea na kuperuzi zaidi.

Akizingumza wakati wa uzinduzi wa ofa hiyo, Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa alisema huduma hiyo imelenga kuwapa wateja uhuru wa kuchagua kifurushi chochote na kufurahia mawasiliano bila kikomo.

“Mawasiliano ya uhakika ni kiungo muhimu katika kuchochea maendeleo hivyo huduma hii ya Halikati itampa mteja uhakika wa mawasiliano ili kusaidia kuendesha shughuli mbalimbali kama biashara, kilimo na uvuvi bila wasi wasi wa kuisha kwa kifurushi chako,” alisema.

Ni dhahiri kuwa shughuli kama kilimo, uvuvi na biashara mbali mbali zikiwemo utalii zinahitaji mawasiliano ili kutafuta masoko, hivyo kuwa muda wa maongezi na intaneti ni muhimu kufanikisha ukuaji na maendeleo ya shughuli hizo.

Aidha, huduma hii ya aina yake katika soko la mawasiliano imelenga pia kupunguza kero mbali mbali ambazo wateja wamekuwa wakikumbana nazo ikiwamo wasiwasi wa kuisha kwa vifurushi pasipo kutumia dakika na intaneti.

Naye, Mkuu wa Biashara wa Zantel, Aneth Muga alisema kupitia ofa hiyo Zantel inahakikisha inampa mteja thamani ya pesa kulingana na matumizi yake.

“Hakuna haja ya kusubiri hadi kifurushi chako kiishe, kupitia ofa hii una uwezo wa kununua kifurushi kipya kabla cha awali hakijaisha na ukaweza kuvusha dakika na Mbs zilizosalia,”alisema Muga.

Vilevile, Ofa hii inampa mteja uwezo wa kuokoa pesa kwani mteja ataweza kupata muda wa maongezi zaidi pamoja na intaneti huku akifurahia huduma bila wasiwasi wa kikomo cha muda wa matumizi.

Kwa kupiga*149*15#, au kujiunga kupitia Wakala wa MIMINA au Ezypesa, mteja wa Zantel kujiunga na kifurushi chochote akipendacho na atakuwa na uwezo wa kuvusha salio la dakika na MBs za intaneti

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.