Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa Atembelea Ujenzi wa Kiwanda Cha Sukari cha Bagamoyo Sugar Limited

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la miwa la  Bagamoyo Sugar Limited linalomilikiwa na Makampuni ya Bakhresa wakati alipotembelea mradi  wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika sukari na shamba la miwa la Kampuni hiyo wilayani Bagamoyo, Agosti 18, 2020. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Bakhresa, Abubakar Bakhresa,  wa tano kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo, Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa na wa nne kushoto ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Makampuni ya Bakhresa , Hussein Sufian
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Makampuni ya Bakhresa, Hussein Sufiani (wa pili kulia) kuhusu kilimo cha miwa wakati  alipokagua ujenzi wa kiwanda cha kusindika sukari cha Bagamoyo Sugar Limited kinachomilikiwa na Makampuni ya Bakhresa wilayani Bagamoyo, Agosti 18, 2020. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Everest Ndikilo na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijionea shughuli mbalimbali za  maabara ya  Bagamoyo Sugar Limited, mali ya makampuni ya Bakhresa ambayo inayojenga kiwanda cha kusindika sukari na kulima miwa wilayani Bagamoyo,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijionea shughuli mbalimbali za  maabara ya  Bagamoyo Sugar Limited, mali ya makampuni ya Bakhresa ambayo inayojenga kiwanda cha kusindika sukari na kulima miwa wilayani Bagamoyo,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa kiwanda cha kusindika sukari  na shamba la miwa la Bagamoyo Sugar Limited, mali ya Makampuni ya Bakhresa, Bagamoyo Mkoani Pwani

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.