Habari za Punde

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFAMASIA DUNIANI








Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  Khalid Masoud Waziri akizungumzia Umuhimu wa Kazi ya Wafamasia katika Maadhimisho ya siku ya Wafamasia Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
 Baadhi ya Wafamasia walioshiriki maadhimisho ya siku ya Wafamasia Duniani wakimsikiliza  Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  khalid Masoud Wazir (hayupo Pichani)  katika ghafla iliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini  Zanzibar.

Mgeni rasmin Mgeni rasmin  Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  Ndg.Khalid Masoud Waziri Katikati akiwa katika picha ya pamoja na Wafamasia  baada ya kumalizika kwa mkutano wa mafunzo .

Picha na Maryam Kidiko -  Maelezo Zanzibar.


Na Kijakazi Abdalla              Maelezo         26/09/2020

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Maalim Abdullah Mzee amewataka wafamasia kufuata maadili ya kazi zao ili kulinda heshima katika kada yao.

Maalim Abdalla ameeleza hayo katika hotuba yake ya siku ya Wafamasia Duniani iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi Mipango,Sera na Utafiti wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo.

Amesema Wafamasia ni moja kati ya kada muhimu katika sekta ya afya ambayo inahitaji watendaji waaminifu na wenye uadilifu katika kutekeleza kazi zao.

Alisema wafamasia wanamchango mkubwa katika jamii ikiwemo kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya dawa katika kukinga na kutibu maradhi mbalimbali .

Aliweka wazi kuwa wafamasia wanawajibu wa kuhakikisha usalama wa dawa kwa wagonjwa wakati wa usambazaji hadi kumfikia mtumiaji.

Kutokana na umuhimu wa kada ya afya, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara y Elimu  amewataka wafamasia, madaktari, wauuguzi na wataalamu wa kada hiyo kushirikiana ili kulinda afya za wananchi.

Amewashauri wafamasia kufikiria njia bora ya kuziendeleza dawa za asili ili kupiga hatua za kimaendeleo kama zilivyo nchi nyengine zikiwemo India na China.

Naye Mwenyekiti  wa Chama cha Wafamasia Zanzibar Bwana Mohammed Kheir amewasisitiza wafamasia kuwa kitu kimoja na kuwa waangalifu katika kutekeleza majukumu yao ili kutoa huduma bora kwa wananchi wenzao.

Siku ya Wafamasia Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 25/09/2020 ya kila Duniani kote na Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Wafamasia na Mabadiliko ya Sekta ya Afya Duniani”.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.