Habari za Punde

Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Waunganishwa Visiwa Vya Unguja na Pemba.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Waziri Kindamba (kulia), akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Miundombinu ya TEHAMA Zanzibar, Mhandisi Shukuru Suleiman baada ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na visiwa vya Unguja na Pemba wakiwa kwenye ukumbi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na usafirishaji, Zanzibar.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa makubaliano wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na visiwa vya Unguja na Pemba wakiwa kwenye ukumbi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Zanzibar. Kushoto ni Katibu wa Wizara hiyo, Dkt. Mustafa Aboud Jumbe.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Waziri Kindamba akiongea na waandishi wa habari kabla ya kutia saini mkataba wa makubaliano wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na visiwa vya Pemba na Unguja wakiwa kwenye ukumbi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar. wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Ndg.Mustafa Aboud Jumbe na Dkt. Zainabu Chaula (wa pili kushoto) wa Wizara hiyo (Sekta ya Mawasiliano), Tanzania Bara.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji  Zanzibar.Ndg. Mustafa Aboud Jumbe akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Wizarani kwake kabla ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa makubaliano wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na visiwa vya Unguja na Pemba. Kulia ni Dkt. Zainabu Chaula wa Wizara hiyo (Sekta ya Mawasiliano), Tanzania Bara

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa miundombinu ya TEHAMA, Zanzibar, Mhandisi Shukuru Suleiman akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Zanzibar kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na visiwa vya Pemba na Unguja.wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. Mustafa Aboud Jumbe, wa pili kushoto ni Dkt. Zainabu Chaula wa Wizara hiyo (Sekta ya Mawasiliano), Tanzania Bara na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri kindamba wa kwanza kulia akisikiliza.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar, Mustafa Aboud Jumbe akiwa ofisini kwake akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) wa Tanzania Bara, Dkt. Zainabu Chaula kabla hawajashuhudia utiaji saini wa mkataba wa makubaliano wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na visiwa vya Unguja na Pemba

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula (wa pili kulia) akiwa ofisini kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar (wa pili kushoto), Dkt. Mustafa Aboud Jumbe kabla ya kushuhudia utiaji saini mkataba wa makubaliano wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na visiwa vya Pemba na Unguja. wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Waziri kindamba akisikiliza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.