Habari za Punde

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM Mhe.Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi Ameomba Kura Kwa Wananchi wa Zanzibar na Kutangaza Vipaumbele Vyake Kwa Wananchi.

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi akitowa maelezi jinsi ya kumpigia Kura katika karatasi ya kura wakati wa mkutano wake wa kufunga kampeni uliofanyika katika uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Jijini Zanzibar na kuomba Kura kwa Wananchi wa Zanzibar na kuwaombea kura Wagombea wote wa CCM kesho katika uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi akisisitiza jambo wakati akitangaza Sera zake baada ya kuchaguli kuiongoza Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, wakati wa mkutano wake wa ufungaji wa kampeni uliofanyika juzi 25/10/2020 katika uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Jijini Zanzibar. na kufungwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.  
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM Mhe.Dkt. Hussein mWinyi akiwahutubia Wananchi wakati wa mkutano wake wa ufungaji wa kampezi za CCM uliofanyika katika viwanja vya Demokrasia Kibanda Maiti Jijini Zanzibar juzi 25/10/2020. na kuwaombe ridhaa zao kumpigia kura kumuwezesha kushinda nafasi ya Urais na kuongoza Zanzibar.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wakimshangilia mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi  akiwahutubia na kuwaomba kura zao na kuwaombea wagombeac Ubunge,Uwakilishi na Udiwani kwa tiketi ya CCM, mkutano huo wa ufungaji wa kampeni za CCM uliofanyika katika Uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Jijini Zanzibar juzi.
Mwenyekiti wa Mstaaf wa CCM na Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Kikwete akihutubia na kumuombea Kura Mgombea Urais wa Zanzibar  Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi wakati wa mkutano wa ufungaji wa kampeni za CCM Zanzibar uliofanyika katika uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Jijini Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein na (kushoto kwa Rais) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Kichama Ndg.Talib Ali Talib, wakifuatilia mkutano wa ufungaji wa kampeni ya CCM iliofanyika uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Jijini Zanzibar.MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwahutubia Wananchi wa Zanzibar katika viwanja vya Demokrasia Kibanda Maiti Jijini Zanzibar wakati wa mkutano wa kufunga kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi ,a kumuombea Kura na kuwaombea Wagombea wote wa CCM.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo wakati akihutubia  katika mkutano wa ufungaji wa kampeni za CCM na kumnadi Mgombea Urais wa Zanzibar na kumuombea Kura pamoja na Wagombea wote wa CCM wa Ubunge, Uwawakilishi na Udiwani, mkutano huo umefanyika katika uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Jijini Zanzibar

UMATI wa Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wakihudhuria mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi uliofanyika katika Uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Jijini Zanzibar.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wakimshangilia mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi  akiwahutubia na kuwaomba kura zao na kuwaombea wagombeac Ubunge,Uwakilishi na Udiwani kwa tiketi ya CCM, mkutano huo wa ufungaji wa kampeni za CCM uliofanyika katika Uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Jijini Zanzibar juzi.
MARAIS Wastaaf wa Tanzania Mhe Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Mrisho Kikwete wakifurahia jambo wakati wa mkutano wa ufungaji wa Kampeni ya Mgombea Urais wa CCM Mhe. Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi, uliofanyika katika uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Jijini Zanzibar 
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi akiteta jambo na Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe.Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, wakati wa mkutano wa ufungaji wa Kampeni za Mgombea Urais wa Zanzibar uliofanyika katika uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Jijini Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.