KATIBU Tawala Mkoa wa
Tanga Judika Omar katikati, akiwaongoza watendaji mbali mbali kutoka Tasaf
makao Makuu na waandishi wa habari, katika kumuombea mwanzilishi wa Tasaf
Tanzania Marehemu Rais Mstaafu Benjamini Wilium Mkapa, wakati wa kikao kazi cha
kuwajengea uwelewa waandishi wa habari kilichofanyika Halmashauri ya Jiji la
Tanga.
MKURUGENZI Mtendaji wa Tasaf Tanzania Ladislaus Mwamanga, akizungumza katika kikao kazi cha kujenga uelewa kwa waandishi wa habari, kuhusu utekelezaji wa kipindi cha Pili cha awamu ya tatu ya Tasaf, huko katika ukumbi wa halmashauri ya jiji la Tanga.
KATIBU Tawala Mkoa wa Tanga Judika Omar akifungua kikao kazi cha kujenga uelewa kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamua ya Tatu ya Tasaf, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf Ladislaus Mwamanga, kikao hicho kilichofanyika halmashauri ya Jiji la Tanga.
MTAALAMU wa
Mawasiliano kutoka Tasaf Zuhura Mdungi, akiwasilisha Madhumuni ya kikao kazi
cha kuwajengea uelewa waandishi wa habari kuhusu PSSN II, kikao kilichofanyika
halmashauri ya jiji la Tanga.
WAANDISHI wa habari
kutoka Pemba, Unguja, Morogoro na Dar Esalam, wakifuatilia ufunguzi wa kikao cha
cha kuwajengea uelewa kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamua ya Tatu
ya Tasaf, kikao hicho kilichofanyika halmashauri ya Jiji la Tanga.
WAANDISHI wa Habari
kutoka Unguja, Pemba na Tanga wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka
Tasaf na katibu Tawala Mkoa wa Tanga Judika Omar, mara baada ya kufungulia kwa
kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu kipindi cha pili cha awamua ya Tatu ya
Tasaf, kikao hicho kilichofanyika halmashauri ya Jiji la Tanga.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, TANGA)
No comments:
Post a Comment