Habari za Punde

Uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Mji Mpya wa Kwahani Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akikata utepe kuzinfungua Nyumba za Kisasa za Kwahani Jijini Zanzibar, na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibare Mhe. Balozi.Mohammed  Ramia Abdiwawa, Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambae pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Dk. Hussein Mwinyi, wakishiriki katika ufunguzi huo uliofanyika leo 12/10/2020
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waBaraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa, akitowa maelezo ya ujenzi wa nyumba za Kwahani Jijini Zanzibar kabla ya kuwela Jiwe la Ufunguzi wa Nyumba hizo leo. 12/10/2020 na (kulia kwa Rais) Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  ambae pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Dk. Hussein Mwinyi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi
Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mshauri Elekezi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Kwahani kutoka Kampuni ya Arqes Africa Ltd ya Jijini Dar es Salaam Bi. Rose Nestory, akitowa malezo wakati akitembelea moja ya nyumba hizo baada ya kuzifungua leo 12/10/2020, na (kulia kwa Rais) Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Mohammed Ramia Abdiwawa, Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambae pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Mwinyi, wakifuatilia maelezo hayo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akitembelea moja ya nyumba 71 za Mradi wa Kwahani baada ya kuzifungua leo 12/10/2020, akiwa na Waziri wa Fedha na Miupango Zanzibar.Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akielekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi baada ya kuzifungua Nyumba za Mradi wa Kwahani Jijini Zanzibar leo 12/10/2020. Na (kulia kwa Rais) Mshauri wa Rais Mhe. Abdulrahaman Mwinyimbegu na (kudshoto kwa Rais) Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa


WANANCHI wa Kwahani Jijini Zanzibar wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Mradi wa Nyumba za Kwahani wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.akihutubia katika hafla hiyo ya ufunguzi(haypo pichani ) ufunguzi huo umefanyika leo 12/10/2020.
MWANANCHI wa Kwahani .Bi. Amina Hassan Abass akisoma risala kwa niaba ya Wananchi wa kwahani wakati wa hafla hiyo ya ufungfuzi wa Mradi wa Nyumba za Kwahani Jijini Zanzibar, zilizofunguliwa leo 12/10/2020 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani )
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Ndg. Khamis Mussa akisoma taarifa ya Kitaalam ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Kwahani Jijini Zanzibar wakati wa ufunguzi wake uliofanyika leo 12/10/2020
WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Mradi wa Nyumba za Kisasa za Kwahani Jijini Zanzibar uliofanyika leo 12/10/2020 katika eneo la mradi huo kwahani
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar ambae pia ni Mgombea Urais Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi, akizungumza na Wananchi wa Kwahani wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mradi wa Nyumba za Kwahani zilizofunguliwa leo 12/10/2020 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein. (hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya ujenzi wa nytumba hizo kwahani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo wakati akiwahutubia Wananchi wa Kwahani wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Nyumba za Mradi wa Kwahani, uliofanyika leo 12/10/2020. Na kuwakabidhi funguo baadhi ya Wakazi wa nyumba hizo
WANANCHI wa Kwahani Jijini Zanzibar wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Mradi wa Nyumba za Kwahani wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.akihutubia katika hafla hiyo ya ufunguzi(haypo pichani ) ufunguzi huo umefanyika leo 12/10/2020.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi funguo mmoja wa wakazi wa nyumba mpya za kwahani Ndg. Ali Hamad Haji, baada ya kuzifungua leo 12/10/2020, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya nyumba hizo kwahani Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi funguo mmoja wa wakazi wa nyumba hizo mpya Ndg. Abdi Ameir Ali, hafla hiyo imefanyika leo 12/10/2020, katika hafla ya ufunguzi wa nyumba hizo uliofanyika katika viwanja nyumba hizo Kwahani Jijini Zanzibar
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.