Mkuu wa chuo cha Kiislamu, Maalim Bakari Chum Ame amewataka Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu cha Kiislamu kudumisha Utamaduni wa Mzanzibar ili kulinda mila, sulka na tamaduni za nchi .
Hayo ameyasema wakati wa maonesho mafupi yanayo husu utamaduni wa mzanzibari ya vyakula na mavazi ya katika ukumbi wa chuo cha kiislamu mazizini mjini Unguja.
Amesema kuendeleza utamaduni wa mavazi kutaifanya jamii kuwa na tabia na hulka Nzuri huku utamaduni wa vyakula vya asili uwafanya kuepukana na maradhi mbalimbali kwa kula vyakula vya asili.
Aidha amewataka wakufunzi na viongozi wa Wanafunzi hao kuendeleza maonyesho hayo kwani yatachangia kukitangaza chuo hicho kupanda daraja zaidi na pia kukuza vipaji vya walimu katika ufundishaji.
Hata hivyo amewataka Wanafunzi kujitahidi zaidi katika masomo yao ili kupata Walimu bora watakao saidia kuongeza ufaulu wa Wanafunzi ili kupata wataalamu bora wa baadae.
Nae msaidizi mkuu wa utawala Ndugu Mohammed Mwinyi Ramadhan amesema kumekuwepo changamoto ya mporomoko wa maadili hali inayo sababisha kila mzee na mtoto wake na hivyo kupelekea kutokea vitendo mbalimbali vya udhalilishaji.
Hivyo amewataka walimu ,Wazazi na Walezi kushirikiana katika malezi ya pamojaa na kulinda tamaduni hizo .
Nae Mkufunzi wa Walimu wa maandalizi na Msingi chini, Mwalimu Shamir Kombo Ali amesema lengo la kuandaa maonesho hayo ni kuwafanya walimu kutambua vifaa na vyakula vya asili ilinao waweze kuwafundisha Wanafunzi wao kwa kukuza utamaduni wa nchi.
No comments:
Post a Comment