Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli Alipozindua Bunge La 12 Jijini Dodoma leo

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi  na (kulia kwake) Mama Mary Majaliwa na na (kushoto kwake) Mke wa Rais Mstaaf wa Tanzania Mama Siti Mwinyi  wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Bunge la 12 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania likizinduliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma leo,13/11/2020.
MARAIS Wastaaf wa Tanzania kutoka kushoto Rais Mstaaf wa Awamu wa Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaaf wa Awamu ya Nne Mhe Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu Mstaaf wa Tanzania Mhe. John Malecela na Makamu wa Rais Mstaaf Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakihudhuria hafla ya ufunguzi wa Bunge la 12 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli akilihutibia leo Jijini Dodoma.
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akilihutubia Bunge la 12 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa hafla ya Uzinduzi wake uliofanyika leo, 13/11/2020 katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.(Picha na Ikulu)

WAGENI waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa Bunge la 12 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Bunge hilo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akilihutubia (hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Naibi Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Akcson, wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Bunge la 12 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akulihutubia na kulizindua leo 13/11/2020.
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana  na kuagana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma leo baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa Bunge la 12  na (kulia kwa Dk.Magufuli ) Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe Ali Hassan Mwinyi na (kushoto kwa Dd. Mwinyi) Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli akimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, baada ya kumalizika kwa hafla ya Uzinduzi wa Bunge la 12 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma leo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.