Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amemuapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Anayeshuhulikia Masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa   Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimuapisha Nd.Rashid Said Rashid   kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshuhulikia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika hafla iliyofanyika  leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa   Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akitia saini hati ya kiapo ya Nd.Rashid Said Rashid  mara baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshuhulikia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika hafla iliyofanyika  leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa   Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimkabidhi  hati ya kiapo ya Nd.Rashid Said Rashid  mara baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshuhulikia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika hafla iliyofanyika  leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa kwa  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshuhulikia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Nd.Rashid Said Rashid  (kutoka kushoto) Waziri wa fedha na Mipango Mhe.Jamal Kassim Ali,Katibu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahya Mzee,Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali na Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid (kulia) Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dk.Mwinyi Talib Haji na Mkuu wa Wilaya ya Mjini pia Kaimu Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe.Marina Joel Thomas (kushoto)  wakiwa katika hafla ya kuapishwa  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshuhulikia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Nd.Rashid Said Rashid, iliyofanyika  leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakiwa katika hafla ya kuapishwa  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshuhulikia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Nd.Rashid Said Rashid, iliyofanyika  leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa kwa  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshuhulikia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Nd.Rashid Said Rashid (hayupo pichani) na kutoka kushoto Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali,Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume.Katibu ORMBLM Ndg.Salum Maulid na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Mhe.Khamis Mussa Omar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa   Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiagana na  Nd.Rashid Said Rashid  mara baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshuhulikia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika hafla iliyofanyika  leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Jamal Kassim Ali na (kulia kwake) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid wakizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Rashid Said Rashid, baada ya kumalizika hafla ya kuapishwa leo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar..,
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Jamal Kassim Ali na (kulia kwake) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Rashid Said Rashid na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Ndg. Khamis Mussa Omar , wakibaduilishana mawazo baada ya kumalizika hafla ya kuapishwa leo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.