Habari za Punde

Wazazi Wametakiwa Kuwa Makini Kufuatilia Nyendo za Watoto Wao.

Na Kijakazi Abdalla                    Maelezo           9/11/2020

JAMII imetakiwa kushirikiana katika kufuatilia nyendo za watoto wao ili kuwakinga na vitendo viovu ambavyo vimeonekana kushamiri kila siku.

Hayo ameyasema Afisa Hifadhi ya Mtoto kutoka Idara ya Wazee na Ustawi wa Jamii Mkasi Abdalla Rajabu huko Mwanakwerekwe katika Mkutano na Waandishi wa Habari wakati akiwasilisha Mada ya Hifadhi ya Mtoto na Malezi.

Amesema watoto wengi wanakumbwa na vitendo viovu kutokana na wazazi kutokuwa makini kwa kutofalia nyendo za watoto hao pamoja  na viashiria vinavyo anza kujitokeza.

Aidha amesema  jukumu la kumlinda mtoto ni la kila mtu ,hivyo amewataka wazazi kuwa na utaratibu wa kuwasiliana  na walimu wa skuli,  madrasa ili kujua mwenendo   matatizo ya watoto wao kwa   kuweza kuyatatua.

Vilevile amesema suala la malezi ni la familia kwani lina jukumu kubwa la kuwaweka watoto kwenye mazingira salama kwa kuwakinga na madhara yeyote yasitokee.

Hata hivyo Afisa huyo amekemea tabia ya wazazi kutengana kwa kupeana talaka kwa wazee hali inayopelekea kutokuwa na mashirikiano madogo baina ya wazazi na watoto kwa kuwaweka kwenye mazingira hatarishi na kukosa haki zao za msingi.

Nae Afisa Mratibu na Malezi Mbadala kutoka SOS Nyezuma Simai Issa amevitaka vyombo vya habari kutoa habari na vipindi vinavyozungumzia njia zinazofikia maendeleo kwa watoto ili viweze kuongoza katika maisha yao.

Mkutano huo wa siku moja umetayarishwa na SOS ambao una lengo la kutoa muamko na vyombo vya habari kwa maendeleo ya jamii husika. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.