Habari za Punde

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akabidhiwa Ofisi

Waziri wa Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo Mh.Tabia Maulid Mwita akipokea Katiba ya Nchi kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Vijana ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Balozi Ali Karume katika Ukumbi wa Wizara ya Vijana Migombani Zanzibar.
Waziri wa Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo Mh.Tabia Maulid Mwita  akitiliana saini na  aliyekuwa Waziri wa Vijana ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Balozi Ali Karume hati ya makabidhiano yamali zinazomilikiwa na Wizara hiyo huko Migombani Zanzibar.

Waziri wa Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo Mh.Tabia Maulid Mwita akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Vijana ,Utamaduni,Sanaa na Michezo baada ya makabidhiano ya Ofisi huko Migombani Zanzibar 

PICHA NA BAHATI HABIB /MAELEZO ZANZIBAR.

Na Mwashungi Tahir   Maelezo     

WAZIRI wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita amesema atahakikisha anafanya kazi kwa mashirikiano ili aweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Ameyasema hayo huko katika Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo katika ukumbi ulioko Migombani wakati wa makabidhiano  na Mh Waziri Mstaafu Ali Karume alipokuwa akimkabidhi ofisi pamoja na vitendea kazi .

Amesema  anaomba mashirikiano ili aweze kufanya kazi zake kwa ufanisi na atatekeleza majukumu yake bila ubaguzi na kuhakikisha Wizara inatimiza malengo yake.

Aidha amesema jukumu hilo la utendaji liwe letu sote ili tuwe na upendo tufikie pahala Wizara tuibadilishe muelekeo.

“Tufanye kazi kwa mashirikiano makubwa ili tuweze kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali kwa kufuata utaratibu uliopangwa,”alisema Waziri Tabia.

Pia alisema napendelea kuona watu wote wanawajibika na kuzingatia misaada ya sheria kwani jukumu letu kutekeleza Ilani kwa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Hata hivyo Waziri Tabia amesema Wizara hii ni muhimu kwa jamii tuchape kazi na kushirikiana na Wizara nyengine kwani kijana anaingia kila sekta miongoni mwao ni Elimu na Utalii.

Nae Waziri mstaafu wa Wizara hiyo Balozi Ali Karume amesema yuko tayari wakati wowote kumpa mashirikiano katika utendaji wa kazi ili lengo lililokusudiwa la Serikali liweze kufanya kazi kwa vizuri.

Amewataka wafanyakazi wa Wizara hiyo kumpa mashirikiano Waziri huyo kama walivyompa yeye ili aweze kufanya kazi zake kwa urahisi zaidi kwa vile na yeye ni kijana

“Natoa ombi kwa wafanyakazi  wenzangu apewe mashirikiano Waziri huyu ili apate urahisi wa kutimiza majukumu yake,”Alisema Balozi Karume.

Kwa upande wake  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo  Amour Hamil Bakari ameahidi kuyafanya yote aliyowaagiza kwa lengo la kutimiza majukumu ya Wizara 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.