Habari za Punde

Makabidhiano ya Afisi ya Katibu Mkuu Kazi Uchumi na Uwekezaji Yafanyika leo

KATIBU Mkuu Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Ndg. Mussa Haji Ali akimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu. Ndg. Salum Maulid Salum (kulia kwake) wakati wa hafla ya kukabidhiana ya Ofisi yaliofanyika katika Afisi ya Katibu Mkuu Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
KATIBU Mkuu Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Ndg.Mussa Haji Ali akisaini hati ya makabidhiano ya Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Ndg, Salum Maulid Salum (kushoto) makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Katibu Mkuu Ikulu Jijini Zanzibar. (Picha na Ikulu)
KATIBU Mkuu Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Ndg.Mussa Haji Ali (kulia) akikabidhiwa Vitendea Kazi vya Ofisi yake wakati wa makabidhiano ya Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Ndg. Salum Maulid Salum (kushoto) hafla hiyo imefanyika katika Afisi ya Katibu Mkuu Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
KATIBU Mkuu Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Ndg. Mussa Haji Ali akizungumza na Wafanyakazi wa Afisi ya faragha wakati wa hafla ya kukabidhiwa ya Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi Rais Ikulu Ndg. Salum Maulid Salum, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Afisi ya Katibu Mkuu Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

 Zanzibar                                                           04.02.2021

KATIBU Mkuu  Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji  Mussa Haji Ali ameeleza umuhimu wa kuendeleza mashirikiano yaliopo kwa watendaji wa Ofisi hiyo kwa azma ya kutekeleza vyema majukumu yao na hatimae kufikia lengo lililokusudiwa.

Hayo aliyasema Ikulu Jijini Zanzibar wakati wa makabidhiano ya Ofisi kati yake na aliyekuwa Katibu Mkuu  wa Ofisi Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum.

Katika hafla hiyo ambapo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Kassim Ali alihudhuria, Katibu Mkuu huyo mpya alieleza kuwa mashirikiano ndio msingi mkubwa wa utendaji kazi.

Alisema kuwa anamatarajio makubwa kwamba kuwepo mashirkiano kati yake na watendaji wa Ofisi hiyo kutasaidia kuimarisha utendaji wa kazi hasa kwa umuhimu wa ofisi hiyo sambamba na kwenda na kasi ya maendeleo iliyokusudiwa.

Aidha, alisema kuwa mbali ya kuwepo kwa mashirikiano suala la mawasiliano miongoni mwa viongozi na watendaji wa Ofisi hiyo ni jambo la muhimu kwani litasaidia katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Kwa upande wake Katibu Mkuu huyo aliahidi kutoa ushirikiano wake kwa viongozi na watendaji wote wa Ofisi hiyo huku akitumia fursa hiyo kumpongeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kumpa ushirikiano wake kabla na baada ya kuteuliwa nafasi hiyo.

Nae aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum alimpongeza Katibu Mkuu huyo mpya kwa kushika wadhifa huo na kueleza kuwa kutokana na uchapakazi wake ana matumaini makubwa kwamba atatekeleza vyema majukumu yake hayo mapya.

Katika maelezo yake Katibu Mkuu huyo aliyemaliza muda wake wa uongozi katika Ofisi hiyo alisisitiza suala zima la ushirikiano na kusema kwamba anamatumaini makubwa kuwa watendaji watampa ushirikiano mzuri Katibu Mkuu huyo mpya kama ule ambao yeye aliupata katika uongozi wake.

Aidha, alitoa pongezi na shukurani kwa watendaji wote kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Ofisi hiyo na kusisitiza kwamba mafanikio hayo yametokana na mashirikiano, umoja, mshikamano na mapenzi kati yao.

Aliwapongeza viongozi wote ambao alifanya kazi nao na kueleza jinsi alivyojifunza mambo kadhaa ambayo yamemsaidia katika utendaji wake wa kazi.

Mapema aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Kassim Ali alimtakia kila la kheri Katibu Mkuu huyo mpya huku akimsisitiza kuendeleza utamaduni wa kushirikiana na watendaji wa  Ofisi hiyo ili mafanikio zaidi yaendelee kupatikana.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.