Na Mwashungi Tahir /Rahima Mohammed 10/2/2021
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema haitasita kutumia mfumo wa utoaji risiti kwa njia ya elektroniki bali kuufanyia marekebisho ili uwze kutumika kwa uhakika.
Akijibu suali la Mhe Machano Othman Said Muwakilishi wa Jimbo la Mfenesini alietaka kujua kuhusu changamoto ya ukusanyaji wa kodi kwa wafanya biashara huko katika Baraza la Wawakilishi Chukwani Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe Jamal Kassim Ali amesema katika kipindi cha majaribio mfumo huo ulibainika kuwa na dosari ambazo zimeanza kufanyiwa marekebisho.
Amefahamisha kuwa mfumo huo wa majaribio umewashirikisha wafanya biashara 150 kutoka makundi tofauti ya biashara Unguja na Pemba.
Waziri Jamal amesema mfumo huo unatarajiwa kuanza kutumika mwezi wa April kwa watu wote waliosajiliwa kulipa kodi na kwamba hivi karibuni itazindua rasmin matumizi ya vifaaa vya mfumo wa kutolea risti za kieletroniki.
Aidha Waziri Jamali amewataka wananchi kudai risiti kila wanapolipa fedha kwa unuuzi wa mafuta ili kuimarisha maendeleo ya nchi na kufikia malengo yake.
Vilevile serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ofisi ya Mufti imekusudia kufanya uhakiki wa misikiti na madrasa zote za Zanzibar ili kuhakikisha misikiti na madrasa inasajiliwa kwa mujibu sheria na taratibu.
Akijibu suala la Mh Salma Mussa Bilali nafasi za wanawake alietaka kujua serikali imejipanga vipi kuhakisha misikiti na madrasa zote Zanzibar zinasajiliwa.
Waziri wa NchiOfisi ya Rais Katiba,Sheria Utumishi na Utwala bora Mhe Haroun Ali Suleiman amesema kwa sasa ofisi hiyo imeshaanza kufanya uhakiki wa madrasa za Mkoa wa Mjini Magharibi na Kaskazini Unguja ambapo zoezi hilo litaendelea Mkoa wa Kusini Unguja na Mikoa yote ya Pemba.
Amesema ofisi hiyo imeeandaa utaratibu wa kufanya ukaguzi wa misikiti na madrasa ili kubaini matatizo yanayozikabili na kuyapatia ufumbuzi kwa kushirikiana na wananchi wenyewe.
Akiuliza suali la nyongeza Mhe Panya Abdalla Nafasi za wanawake alilouliza kwanini walimu wa madrasa baadhi yao hawana taaluma ya kutosha na katika kusomesha na kutaka kujua ofisi hiyo imejipanga vipi.
Waziri Haroun amesema Ofisi ya Mufti imejipanga vzuri katika kuwapa elimu ili kupata walimu bora katika ufundishaji.
Akijibu suala la Mhe Abdallah Abas Wadi Jimbo la Nungwi kutokana na changamoto ya kukosekana kwa maji safi katika Kijiji cha Nungwi na Fukuchani Waziri wa Maji nishati Suleiman Masoud Makame amesema ZAWA inaendelea na zoezi hilo kwa kushirikiana na viongozi wa siasa wajimbo la Nungwi na Mkoa na wasamaria wema ili kuharakisha huduma hiyo ipatikane vyema.
Aidha kupitia Wizara ya Maji na Nishati imesema ZAWA inaendelea na zoezi la kupitia mtandao wa maji kutoka katika vyanzo vitatu vinavyohudumia eneo la Nungwi kwa kusawadhisha mivujo mingi inayotokana na hujuma za watu mbalimbali pamoja na kuondoa bomba zilizoharibika kwa lengo kuwafikia wananchi.
Wakati huohuo wajumbe wa Barza la Wakilishi wamewachagua wabunge watano kuenda kushiriki katika Bunge la Jamuhuri ya MUUngano wa Tanzania ambao ni Ameir Abdallah Ameir,Mwantatu Mbarak Khamis,Bakari Hamadi Bakar,Suleimani Haroub Suleiman na Bahati Khamis Kombo.
Vilevile Baraza limechagua wenyeviti wa Baraza Mwanasha Khamis Juma na Shabani Ali Othamani,pia limewachagua viongozi wa umoja wa wawakilishi wanawake ya Baraza la Wawakilishi (UWAWAZA) ambapo Mwenyekiti Sada Mkuya Salum,Makamo mweyekiti Mwantatu Mbaraka Khamis.
Aidha Anna Athanas Paul kuwa katibu wa umoja huo, mtunza hazina Panya Ali Abdallah pamoja na wajumbe wakamati tendaji ya UWAWAZA Bahati Khamis Kombo,Salha Mohd Mwinjuma,Rukia Omar Mapuri na Mwanajuma Kassim Makame.
No comments:
Post a Comment