Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi Amemtembelea Kizuka Bi. Aweina Seif.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mjane wa Marehemu aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.Bi.Aweina Seif, alipofika nyumbani kwao Mbweni Wilaya ya Magharibi "B"Unguja kumtembelea leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua na Familia ya Marehemu aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ikisomwa na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume, alipofika nyumbani kwa marehemu Mbweni kumtembelea Mjane wa Marehemu Bi. Aweina Seif leo 26-2-2021.  

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi alifika nyumbani kwa kizuka wa Marehemu Seif Sharif Hamad huko Mbweni na kuonana nae pamoja na familia yake na ya Marehemu huku akitumia fursa hiyo kumuomba kizuka pamoja na wanafamilia kuwa na subira na Mwenyezi mungu atawafanyia wepesi.

Akiwa huko nyumbani kwa Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad ambapo Mama Mariam Mwinyi na Alhaj Dk. Mwinyi, Rais Dk. Mwinyi alimuahidi kizuka huyo kwamba ataendelea kushirikiana nae wakati wote yeye pamoja na Serikali anayoiongoza.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.