Habari za Punde

Kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda Biashara na Mazingira Imetembelea Kiwanda cha Kuchakata Chai Uniliver Tanzania na Kusikiliza Changamoto za Wafanyakazi na Wafanyabiashara Katika Mkoa wa Iringa.

Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira huku wakiwa wameambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe (Mb) pamoja na Naibu Waziri Mhe. Exaud Kigahe (Mb) wakisikiliza taarifa na maelezo kutoka kwa Johnson Muhavile Meneja mkuu wa kiwanda cha chai cha Uniliver (UTTL) cha Lugoba kilichopo wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa
Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira huku wakiwa wameambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe (Mb) pamoja na Naibu Waziri Mhe. Exaud Kigahe (Mb) wakikagua na kujionea utendaji kazi wa kiwanda cha chai cha Uniliver (UTTL) cha Lugoba kilichopo wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa. Tarehe 14, Machi 2021.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe, David Kienzile (Mb) akiwa ameongoza kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira huku wakiwa wameambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe (Mb) pamoja na Naibu Waziri Mhe. Exaud Kigahe (Mb) wakiwasili kwenye kiwanda cha chai cha Uniliver (UTTL) cha Lugoba kilichopo wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa. Tarehe 14, Machi 2021.Picha Zote na Eliud Rwechungura.

Na.Eliud Rwechungura.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe, David Kienzile (Mb) ameongoza kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira huku wakiwa wameambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe (Mb) pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) kutembelea kiwanda cha Kampuni ya Uniliver (UTTL) cha Lugoba kilichopo wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

Katika ziara hiyo iliyofanyika Machi 14, 2121 Waziri wa Viwanda na Biashara na kamati ya bunge wametembelea kiwanda hicho na kuona uzalishaji wa chai ukiendelea katika kiwanda hicho kinachochakata chai tani 100 kwa siku huku kikiwa kimetoa ajira za kudumu 171 pia kiwanda kimetoa ajira ambazo sio za moja kwa moja.

Kiwanda hicho kina mashamba yenye ukubwa wa hekta 3,457 yanayotumika kwa ajili ya kilimo cha chai kwa ajili ya Kiwanda hiki. Aidha kiwanda hiki cha kuchakata chai cha Lugoba kina uwezo uliosimikwa wa kuzalisha chai ni kilogram 100,000 kwa siku ambapo uzalishaji kiwanda kwa mwezi Januari – Mei ni kilogramu 100,000 kwa siku, mwezi June - septemba ni kilogram 50,000 kwa siku na kwa kipindi cha Oktoba – Disemba ni kilogram 80,000 kwa siku amabapo kiwanda hiki huuzwa ndani ya nchi kwa wateja wao ambao ni Afritea, Chai bora n.k na pia wana masoko nje ya nchi.

Kamati ya kudumu ya bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imepata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara, na wakulima wa chai na wazalishaji wa mbao wa Wilaya tatu za Kilolo, Iringa Mjini na Mufindi ambao walikusanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafinga ili kueleza changamoto zao ambazo ni ubovu wa barabara, kodi na umeme.

Waziri Mwambe, amesema kuwa Rais Magufuli anataka kutengeneza mabilionea hivyo amepokea maoni yote yaliyotolewa na kuahidi kuyafanyia kazi hasa TBS kuratibu kutengeneza viwango vya bidhaa, aidha Waziri Mwambe ameiagiza TBS mkoa wa Iringa kukaa na kutengeneza viwango vya ubora wa bidhaa katika mkoa wa Iringa, aidha amewaomba wananchi wa Mkoa wa Iringa kuendelea kuchapa kazi kwani Serikali imezisikia changamoto zao zote hivyo zitafanyiwa kazi kwa haraka ili kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara ambayo ndio lengo kuu la Wizara.

Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema kuwa huu ni Mkoa wake ni lazima apambane katika kutatua changamoto za wafanyabiashara wa Mkoa wa Iringa, Aidha amewaomba wafanyabiashara kutokukwepa kodi ili kuiwezesha serikali kutatua changamoto zao na pia watumishi wa serikali kutumia vizuri fedha za serikali.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati, Mhe, David Kienzile Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Mkoani Iringa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira amesema kuwa kamati imepokea changamoto zote za Kiwanda cha Uniliver na wafanyabiashara katika kuhakikisha zinafanyiwa kazi kwa haraka ili kurahisha biashara katika ukanda huu ambao unachangia kodi ya serikali Zaidi ya Bilioni 35.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.