Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akielekea katika
ukumbi wa Mikutano wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa ajili ya kupokea
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kwa mwaka wa
Fedha 2019/2020 leo tarehe 28 Machi 2021.
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere akionesha moja ya
Taarifa zake za ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20 kabla
ya kuziwasilisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan leo tarehe 28 Machi 2021 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere wakati akitolea
maelezo moja ya Taarifa zake za ukaguzi leo tarehe 28 Machi 2021 katika Ikulu
ya Chamwino mkoani Dodoma.
Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga mara baada ya kutoka katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu ya Chamwino.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment