GARI Maalum la JWTZ lililoandaliwa kwa ajili ya kubeba Mwili wa Hayati John Pombe Magufuli ukiwasili katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar, ukizungumka Uwanja baada ya kuwasili kwa ajili ya hafla ya kuaga kwa Wananchi wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama na Viongozi wa jukwaa kuu wakati mwili wa Hayati John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwasili katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar kwa ajili ya kuagwa na Wananchi wa Zanzibar.
MAKAMANDA wa Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ
wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa hayati John Pombe Magufuli
walipowasili Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar kwa ajili ya kutowa heshima za
mwisho kwa Wananchi wa Zanzibar katika uwanja hivyo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa
Taifa, katika hafla ya kuuaga mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika
uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar, na (kulia kwa Rais) Waziri Mkuu wa Tanzania
Mhe.Kassim Majaliwa na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakipiga
saluti wakati ukipigwa wimbo wa Taifa katika hafla ya kumuaga Hayati Dkt. John
Pombe Magufuli katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakipiga
saluti wakati ukipigwa wimbo wa Taifa katika hafla ya kumuaga Hayati Dkt. John
Pombe Magufuli katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya mazishi Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza
kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kuzungumza na Wananchi katika hafla ya kuuaga mwili
wa Hayati Dkt.Jon Pombe Magufuli katika uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Zanzibar katika
hafla ya kuuaga mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania , hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Amaan
Jijini Zanzibar
WANANCHI wa Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi
(hayupo pichani) akihutubia wakati wa hafla ya kuuaga mwili wa Hayati Dkt.John
Pombe Magufuli, aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hafla hiyo
imefanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar
WANANCHI wa Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi
(hayupo pichani) akihutubia wakati wa hafla ya kuuaga mwili wa Hayati Dkt.John
Pombe Magufuli, aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hafla hiyo
imefanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini ZanzibarRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akitowa heshima za mwisho kwa mwili wa
Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania, wakati wa hafla ya kumuaga marehemu katika Uwanja wa Amaan Jijini
Zanzibar leo 23/3/2021
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi
akitowa heshima za mwisho kwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hafla hiyo ya kumuaga imefanyika katika
Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.
No comments:
Post a Comment