Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Awatembelea Majeruhi Waandishi wa Habari wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Waliopata Ajali leo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Hospitali ya Mnazi Mmoja kuwatembelea na kuwajulia hali Waandishi wa habari wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, waliopata ajali wakiwa katika msafara wa ziara katika Mkoa wa Kusini Unguja na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimjulia hali Mwandishi wa habari wa Makamu wa Pili wa Rais Ndg. Kassim Abdi, na kupata maelezo kutoka kwa Daktari Amour Suleiman alipofika Hospitali ya Mnazi mmoja kuwatembelea na kuwajulia hali majeruhi wa ajali hiyo iliotokea katika maeneo la Kitongani Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika ziara ya kizazi na  (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na (kulia kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimjulia hali Mpiga Picha wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Bw.Hassan Issa, alipofika Hospitali ya Mnazi Mmoja kuwatembelea na kuwajulia hali majeruhi wa ajali hiyo iliotokea katika eneo la Kitogani Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika msafara wa Makamu wa Pili wa Rais. na (kulia kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiondoka katika viwanja vya hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kumaliza kuwakagua na kuwapa pole Waandishi wa habari wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, waliopata ajali katika eneo la Kitogani wakiwa katika msafara wa ziara katika Mkoa wa Kusini Unguja, akiwa na Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar  Mhe.Nassor Ahmed Mazrui na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.