Habari za Punde

Wilaya 10 za Unguja na Pemba Wapata Mafunzo ya Utekelezaji wa Mradi wa Kilimo cha Viungo.

Afisa kutoka mradi wa Viungo anaehusika na maswala ya vikundi vya kuweka na kukopa.Bi. Agness Nicodemas akitoa ufafanuzi katika mafunzo ya siku tano wa wasimamizi wa vikundi hivyo ambavyo lengo kuu nikuwajengea uwezo namna bora ya kusimamia vikundi vyao.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ya siku tano kutoka shehia 16 za Unguja wakifuatilia kwa makini utolewaji huo wa elimu ambalo unalenga kuwajengea uwezo.

Na Muhammed Khamis.

Kwa lengo la kuhakikisha ufanisi zaidi unapatikana kupitia utekelezaji wa mradi wa viungo viongozi 26 wa vikundi vya kuweka na kukopa (CRP) wamepatiwa elimu juu ya namna bora ya kuwafundisha wanachama wao ili waweze kusimamia vikundi vya kuweka na kukopa katika shehia zao.

Utolewaji wa mafunzo hayo umekuja kufuatia utekelezaji wa mradi wa viungo ambao unajikita na maswala ya kilimo cha mboga mboga,matunda pamoja na viungo katika kupitia wilaya 10 za Unguja na Pemba.

Awali akitoa mafunzo hayo Afisa kutoka mradi wa viungo  anaehusia na maswala ya vikundi vya kuweka na kukopa Agness Nicodemas alisema kwa kuwa mradi huo wa viungo una sehemu ya kutoa mkopo kwa vikundi wameona ipo haja kabla ya kupewa mikopo hio wanufaika kupatiwa elimu kabla.

Alisema elimu ndio jambo pekee ambalo litawawezesha wanaufaika kupata mikopo na kuitumia vizuri mikopo hio hatimae waweze kuirejeshe kwa muda muafaka pamojam na kujiongezea kipato.

Sambamba na hayo viongozi hao wa vikundi waliaswa kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa usimamizi wa vikundi kwa lengo la kuhakikisha vikudi hivyo vinakua imara zaidi.

Kwa upande wake mtalamu wa maswala ya vikundi  vya kuweka na kukopa kutoka TAMWA-Z’bar Muhidini Ramadhani aliwataka viongozi hao wa vikundi (CRP)kuhakikisha kuwa hawafanyi shughuli zao bila ya kuwa na katiba.

Alisema ili viukundi vya kuweka na kukopa viweze kufanya kazi zake vizuri bila ya migogoro yoyote hile ni lazima kuwepo na katiba ambayo itaweka kila kitu wazi ikiwemo masharti ya wanachama ni kwa namna gani wataweza kukopa fedha na kurudisha.

Hata hivyo Afisa huyo aliwataka viongozi hao wa vikundi hivyo kuwafahamisha wanachama wao kutumia mikopo wanayochukua kwa melengo waliojiwekea na sio kutumia fedha hizo kwa mambo ambayo yatawafanya wasiweze kurudisha fedha hizo za mkopo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ya siku tano walisema mafunzo hayo yamekuja muda muafaka ambapo wana vikundi wengi hawakua na elimu kuhusu utaratibu mzuri wa kuweka na kukopa.

Faida Mohammed Shaibu kutoka Shehia ya Kianga wilaya ya magharib A Unguja alisema kwa muda mrefu amekua kiongozi wa kikundi na amekua akikutana na chanagamoto ambazo wakati mwengine alishindwa kuzitatua kwa kukosa elimu sahihi.

Alisema kupitia mafunzo hayo sasa yamemjenga vyema na anaamini kwamba atakua msimamizi mzuri sambamba na kutoa elimu stahiki kwa wanachama.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.