Habari za Punde

Kamati ya Makatibu Wakuu Yaandaa Mkakati Kabambe Kuboresha Michezo Mashuleni.

Kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara zenye dhamana yaElimu,Michezo na TAMISEMI  wakiwa kwenye kikao kazi leo Aprili 27,2021 Jijini Dodoma kujadili utekelezaji wa maelekezo ya Mawaziri wenye dhamana hizo hizo kwa lengo la   kuandaa Mkakati wa Utekelezaji wa masuala mbalimbali ya uimarishaji wa somo la Elimu kwa Michezo na Michezo katika shule za Msingi na Sekondari hapa nchini chini ya uenyekiti wa Prof.Riziki Shemdoe ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya  TAMISEMI.
Dkt. Hasssan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia eneo la Elimu ndugu  Gerard Mweli (kulia) wakihudhuria kikao cha Kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara zenye dhamana ya Elimu, Michezo na TAMISEMI  wamefanya kikao kazi leoAprili 27,2021Jijini Dodoma kujadili utekelezaji wa maelekezo ya Mawaziri wenye dhamana hizo hizo kwa lengo la   kuandaa Mkakati wa Utekelezaji wa masuala mbalimbali  yauimarishaji wa somo la Elimu kwa Michezo na Michezo katika shule za Msingi na Sekondari hapa nchini. Upande wa pili ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Yusufu Omary Singo.

Na John Mapepele, Dodoma.

Kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara zenye  dhamana ya Elimu, Michezo na TAMISEMI  wamefanya kikao kazi leo Aprili 27,2021 Jijini Dodoma kujadili  utekelezaji wa maelekezo ya Mawaziri  wenye dhamana hizo hizo kwa lengo la   kuandaa  Mkakati  wa Utekelezaji wa masuala  mbalimbali  ya uimarishaji wa somo la Elimu kwa Michezo na Michezo katika shule za Msingi na Sekondari  hapa nchini


Mwenyekiti wa Kikao hicho, Prof.Riziki  Shemdoe  ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI amesema  miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa  na kukamilika ni pamoja na   kuandaliwa kwa  mapendekezo ya uimarishaji wa ufundishaji wa somo la michezo shuleni na tahasusi zenye somo hilo kwa kidato cha tano  ambapo ameseme tahasusi hizo zitaanza kufundishwa katika mwaka huu wa masomo.


Pia rasimu ya Mpango Mkakati na Mikakati ya utekelezaji wa masuala mbalimbali ya  somo  la Elimu kwa michezo na michezo katika shule za Msingi na Sekondari  imeandaliwa ili  kuboresha  michezo mashuleni.

Kuhusu kuandaa kiunzi cha uendeshaji wa michezo ya UMITASHUMTA na 


UMISSETA  Prof. Shemdoe amesema  tayari  Kamati ya Wataalam imeshauri kuwa  kwa sasa  miongozo iliyopo itumike na kiunzi tayari kimeshaandaliwa kwa kuzingatia changamoto  zilizopo ambapo  kitajadiliwa  na wadau wote Juni mwaka huu wakati wa michezo ya UMISHUMTA NA UMISSETA na  kwa sasa tayari miongozo hiyo imeshatumwa kwenye  mikoa yote hapa nchini.


Aidha, suala la uundwaji wa Kamati ya kitaifa ya UMISHUMTA NA UMISSETA tayari imependekezwa na kukubalika kuundwa kwa Kamati ya Usimamizi itakayoundwa na wataalam wawili wawili kutoka kwenye kila Wizara ambapo imekubalika kuwa  pamoja na usimamizi, Kamati itatumia fursa hiyo kujifunza na kuangalia changamoto zilizopo kwenye uendeshaji wa michezo ya UMITASHUMTA  na UMISSETA kuandaa  mapendekezo yatakayojadiliwa  na wadau wote kwa ajili ya  maboresho zaidi.


Prof. Shemdoe amesema kuhusu mchakato wa maandalizi ya UMISHUMTA NA UMISSETA mwaka huu, tayari mikoa yote imeshaandikiwa barua ya taarifa na Mhe. Waziri Ofisi ya Rais –TAMISEMI na kwamba waratibu wa michezo wanakwenda kwenye ukaguzi wa viwanja na maeneo ya malazi na chakula kuanzia Aprili 28-30, mwaka huu. Pia Kamati ya wataalam inaendelea na ufuatiliaji wa Shule teule za michezo ili kuhakikisha kuwa michezo inafanyika kwenye kiwango kinachotakiwa.


Makatibu Wakuu walioshiriki  kwenye  kikao hiki ni pamoja Mwenyekiti wa kikao hicho, Prof. Riziki  Shemdoe  ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI,na Naibu wake  anayeshughulikia eneo la Elimu ndugu  Gerard Mweli, mwingine ni  Dkt. Hasssan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Dkt. Leonard Akwilapo  kutoka  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojioa pamoja na Watendaji mbalimbali kutoka  Wizara hizo.


Maelekezo  ya Mawaziri wenye dhamana ya elimu, Michezo na TAMISEMI yalitolewa wakati wa kikao cha pamoja kilichofanyika Februari 8, Mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.