Habari za Punde

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said Ameupongeza Uongozi wa Skuli ya Kijamii ya International ya Zanzibar kwa kufanya bidii na kuhakikisha Skuli yao inakua bora barani Afrika.Na Maulid Yussuf WEMA ZANZIBAR

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said ameitaka jamii kuchangamkia fursa zinazotolewa na wadau mbalimbali wa elimu ili waweze kufikia malengo yao.

Ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa  udhamini wa masomo kwa  Wanafunzi wenye asili ya Kizanzibari wenye  vipaji  anaetoka katika familia yenye hali duni, kupitia Skuli ya kijamii ya International ya Zanzibar huko Mbweni mkoa wa mjini magharibi Unguja.

Amesema  kufanya hivgo kutawasaidia wazazi katika kupungukiwa na.gharama katika suala zima la ulipatu wa ada hasa wanaotaka kusoma nje ya nchi.

Amesema ni jambo zuri kuishirikisha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu kwa  kuwatangazia fursa za masomo zinazopatikana katika Skuli hiyo ili kuhakikisha Zanzibar inazalisha wataalamu wazalendo.

Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea  kushirikiana na wadau mbali mbali hasa katika sekta ya elimu ambapo inasaidia kwa kiasi kikubwa kupata fursa mbalimbali hasa za kielimu.

Aidha Mhe Said ameupongeza uongozi wa Skuli ya kijamii ya   International  ya Zanzibar kwa kufanya bidii na kuhakikisha  Skuli yao inakua  bora barani Afrika.

Amesema uwepo wa Skuli hiyo nchini  husaidia  Wanafunzi  kufahamu mazingira na tamaduni za watu kutoka Mataifa mbalimbali duniani.

Mhe Waziri ameitaka jamii kuondokana na fikira za kuwa Skuli hiyo ni ya watu wenye kipato cha juu  bali ni kwa ajili  watu wote kutoka ndani ya nje na nje ya nchi.

Aidha mhe Simai amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kujenga Skuli za ghorofa ili kupunguza changamoto ya  uchache wa madarasa katika Skuli zake.

Aidha ameiomba jamii nayo kuwa tayari kuisaidia Serikali  kwa kuhakikisha watoto wanapata malezi mazuri kwa kushirikiana na wazazi na Serikali ili watoto waweze kutimiza ndoto zao.

Nae mwenyekiti wa bodi ya wazazi  Skuli ya Kijamii ya International ya Zanzibar bi Vyonne Karume  amesema malengo ya Skuli hiyo ni  kuhakikisha wanakua na wahitimu watakaoleta mabadiliko ya kiuchumi katika Mataifa yao na hata  dunia nzima. 

Amesema  inahakikisha inatoa  Wanafunzi na  wanapata nafasi za kuendelea na masomo yao ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali duniani.

Amesema Mwanafunzi atakaebahatika kupata udhamini huo atajumuika na wanafunzi wenziwe kwenye shughuli zote za Skuli na udhamini huo utadumu kwa muda wote wa masomo hadi atakapo maliza kidato cha sita. 

Zaidi ya shilingi milion 32 zitatumika kwa kila mwaka ili kumdhamini mwanafunzi mmoja ambapo udhamini huo utakuwa ni wa miaka 4  kwa kuchukua mwanafunzi mpya kila mwaka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.