Habari za Punde

Benki ya NMB Yazindua Mpango wa Uwezeshaji wa Fursa za Mikopo kwa Madereva wa Bajaji na Bodaboda "NMB Mastabodo – Miliki Chombo”

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimpungia mkono Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna, akiwa amepakiwa kwenye pikipiki na mwendesha Bodaboda mara baada ya kuzindua rasmi fursa ya mikopo kwa madereva Bodaboda na Bajaji kupitia NMB MASTABODA – MILIKI CHOMBO.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akizungusha bango kuashiria uzinduzi wa mpango wa uwezeshaji wa mikopo kwa madereva Bajaji na Bodaboda ijulikanayo kwa NMB MASTABODA – MILIKI CHOMBO. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna (wa pili kutoka kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Madereva Bodoboda Bw. Michael Massawe na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati Benki ya Nmb, Bw. Filbert Mponzi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na (kushoto kwake) Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna (katikati) akikabidhi funguo kwa dereva bodaboda ambaye amenufaika na mkopo wa NMB MASTABODA – MILIKI CHOMBO.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna akifafanua jambo kuhusu fursa ya mikopo inayotolewa na benki hiyo wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa “NMB MASTA BODA – MILIKI CHOMBO”, mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati Benki ya Nmb, Bw. Filbert Mponzi akieleza jambo wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Ubungo Plaza, Jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa mpango wa uwezeshaji wa fursa za mikopo kwa madereva Bajaji na Bodaboda ijulikanayo kwa NMB MASTABODA – MILIKI CHOMBO iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Ubungo Plaza, Jijini Dar Es Salaam.
Sehemu ya Wauzaji wa pikipiki aina ya Boxer na Bajaj wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya Madereva Bajaji na Bodaboda walioshiriki katika hafla hiyo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akifurahia jambo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna (kushoto). Kulia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati Benki ya Nmb, Bw. Filbert Mponzi.
Msanii wa nyimbo za Singeli, Dulla Makabila akiimba nyimbo na kucheza na baadhi ya Madereva Bodaboda na Madereva Bajaji walionufaika na fursa hiyo wakati wa uzinduzi wa hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.