Habari za Punde

WAZIRI AISISITIZA CHAMA CHA SOKA NCHINI (TFF) KUWEKEZA NGUVU KATIKA MAENEO NCHINI BAADA YA MRADI KITUO CHA MICHEZO KIGAMBONI NA TANGA KUISHA

 

Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Inocent Bashungwa akiwa katika ziara ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Michezo cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam akiwa na Maafisia wa TFF.
Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Inocent Bashungwa  akipata maelezo ya Mradi wa Kituo cha Michezo kutoka kwa Mwenyekiti wa TFF wakati wa ziara yake kutembelea Mradi huo ulioka katika eneo la Kigamoboni Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Inocent Bashungwa akipata maelezo ya michoro ya Ujenzi wa Kituo hicho cha Michezo kinachojengwa katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake kujionea ujenzi huo.


Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa inocent Bashungwa amefanya Ziara katika Mradi wa Kujenga Kituo cha Michezo cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF ulioko Kigamboni Kibada Jijini Dar es Salaam.

 

Waziri Bashungwa amefanya ziara hiyo leo akiwa ameongozana na Rais wa Shilikisho la Mpira wa Miguu Wallec Karia amekagua Mradi huo unaofadhiliwa na Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) Nchini Tanzania ambao Umefanyika Kigamboni Dar es Salaam na Jijini Tanga, Waziri ameshuhudia Shuguli za Ujenzi zinavyoendelea na kujiridhisha na kutoa hari kwa Uongozi kufanikisha zoezi kwa kasi kwalengo la kumaliza kujenga viwanja Vinne mapema Mwisho wa Mwaka Huu.

 

Waziri ameisitizia TFF kwa awamu inayokuja ya fungu kutoka FIFA kuwekeza katika Maeneo mengine Nchini kwa kiwango kile kile kama Mradi wa Kigamboni na Tanga kwa kuzingatia hali ya kijiografia ya nchi yetu ili kutonyima fursa ya kujiendeleza kimichezo kwa Wananchi waishio mbali na Dar es Salaam na Tanga.

 

Kwa upande wa TFF Rais Karia aliorodhesha baadhi ya Huduma za kimicheo zitakazo kuwa zinapatikana hapo ambayo ni Mpira wa Miguu kwa viwanja vya Nyasi Bandia na Nyasi za Kawaida, Hoteli ya Hadhi ya Nyota Tatu, Hostel kwa Wakufunzi w Michezo na Wanamichezo, Viwanja vya mpira wa Wavu na Pete pia Kutakuwa na Mabwawa ya Kuogelea kwaajili ya Kuwanoa Wanamichezo wa Kuogelea Nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.