a.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, akitunukiwa Tuzo ya Shukrani kutoka kwa
viongozi na wanachama wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano
Serikalini (TAGCO) kwa mchango wake aliotukuka kwenye kuleta mageuzi katika sekta
ya habari nchini.
a.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akiongoza kikao kazi cha Maafisa
Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini Jijini Mbeya, kushoto ni Naibu wake
Dkt. Ally Possi, kulia ni Katibu
Mkuu -TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe
Na John Mapepele, Mbeya
Akikabidhi
tuzo hiyo kwa Dkt. Hassan Abbasi, Mwenyekiti wa TAGCO, Paschal Shelutete wakati
wa kikao cha 16 cha TAGCO kilichofanyika Jijini Mbeya Mei 24,2021 amesema Dkt. Abbasi
ametoa mchango mkubwa akiwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Mkuu wa
Serikali tofauti na hapo awali.
“Ni
katika kipindi hiki ambapo miradi ya kimkakati ya Serikali ilisemewa vizuri zaidi
na kufahamika na watu wengi hivyo kuwafanya wananchi kuipenda Serikali yao” Amefafanua
Shelutete.
Ameongeza
kwamba Dkt. Abbasi amefanikiwa kusimamia tasnia ya Habari na uboresha mahusiano
ya kikazi miongoni mwa wadau wote wa Sekta ya Habari.
kwa
upande wake Dkt. Abbasi amewashukuru Waandishi kwa kumpa tuzo hiyo na kuahidi
kuendelea kuwapa ushirikiano ili waweze kuendelea kutekeleza majukumu wao
kikamilifu kwa nafasi yake ya sasa ya Katibu Mkuu. Wizara ya Habari, Utamadunim
Sanaa na Michezo.
“Tuendelee
kushirikiana katika cheo hiki kipya cha Katibu Mkuu katika Wizara yetu ambayo
ni Wizara muhimu inayogusa umma kwa nyanja ya burudani na huzuni kutokana na
Sekta zake” Ameongeza Dkt. Abbasi.
Amewataka Waandishi kuzingatia weledi wakati wote wa undaji wao
wa kazi ambapo amesisitiza kwamba Serikali inatambua mchango wa waandishi na
kwamba itaendelea kuhakikisha sekta inaboreka na kuchangia kwenye uchumi wa Taifa.
Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania. Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumwamini na kumrejesha tena kwenye nafasi ya Katibu Mkuu na kuahidi kufanya kazi kwa weledi na bidi ili kutekelea Ilani ya Chama cha
Mapinduzi na maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia.
Kikao
hiki kimefunguliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.
Innocent Bashungwa kimehudhuriwa na Naibu wa Wizara hiyo, Katibu Mkuu -TAMISEMI
Prof. Riziki Shemdoe ambaye ametoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya
kiutumishi kwa maafisa Habari kutoka halmashauri zote nchini,na viongozi
mbalimbali wa Serikali na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali zaidi ya 270.
No comments:
Post a Comment