Habari za Punde

TAMWA-ZNZ yawakutanisha wadau 60 wa kupambana na udhalilishaji

Afisa ufuatiliaji na tathmini TAMWA-ZNZ Mohammed Khatib akifungua kongamano la siku moja la wadau wa kupambana na udhalilishaji Zanzibar katika ukumbi wa TAMWA uliopo Wilaya ya kati Unguja.
Hakimu wa Mahakama ya Mkoa Vuga mjini Unguja Valentina A.Katema akitoa ufafanuzi wa mdai mbali mbali yanayoonekana kuwa kikwazo katika kesi mbali mbali za udhalilishaji ikiwemo sula la ushahidi.
Mwanasheria kutoa ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka DPP Khamis Juma alipokua akiendesha majadiliano ya siku moja kwa wadau wa kupambana na udhalilishaji.
Mmoja katika washiriki na wadau wa udhalilishaji akichangia jambo katika kongamano la siku moja la wadau wa kupambana na udhalilishaji Zanzibar katika ukumbi wa TAMWA uliopo Wilaya ya kati Unguja


 

Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ


 

Baadhi ya wazanzi na walenzi ambao watoto wao waliwahi kufanyiwa  kadhia ya udhalilishaji wa kijinsia wamesema hawaridhishwi na utaratibu wa mwenendo wa kesi zao katika vyombo mbali mbali vya sheria na kwamba wanaamini wakati mwengine hucheleweshwa kwa makusudi ili kuondoa ushahidi.


 

Waliyasema hayo kwa nyakati tofauti katika ukumbi wa ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari zilizopo TAMWA Tunguu Wilaya ya kati Unguja katika mkutano maalumu wa majadiliano uliolenga kutazama chanagamoto za matukio hayo na njia bora za kupunga au kumaliza kabisa.


 

Mmoja miongoni mwa wazazi ambae jina lake limehifadhiwa alisema anasikitishwa sana hadi sasa watoto wake wanne wamebakwa na kinachomuumiza zaidi anaefanya matukio hayo ni baba yao wa kambu.


 

Alisema wakati matendo hayo yakiendelea Baba yao wa kambu alimzuia mke wake kutotoa taarifa hizo nje na alimpa fedha hatimae mama huyo aliamua kunyamaza kimya bila kutoa taarifa kilichokuja kusaidia kugundulikana kwa taarifa za matukio hayo ni walimu wa skuli ambao wanawasomesha watoto hao baada ya kuona mwenendo usikua wa kawaida kwa wanafunzi hao.

 

 

Hata hivyo alisema kwa sasa kesi hio haiendelei na haoni kama kuna taaswira ya haki kutendeka kwani amekua akizungushwa huku na kule jambo ambalo anaamini hwenda ni mpango wa makusudi kuvuruga kesi hio.


 

Akitoa ushuhuda mzazi mwengine ambae pia jina lake linahifadhiwa alisema kesi ya kubakwa kwa mtoto wake ipo Mahakamani tangu tarehe  27/2/2021 lakini hadi leo hii bado hajaitwa kutoa ushahidi bali alieitwa ni yule mtuhumiwa pekee na hana taarifa za undani zaidi kuhusu kesi hio licha ya kuwa yeye ndio alifika katika vyombo vya sheria  kutoa malalamiko.


 

Sambamba na hayo alisema mtu alietuhumiwa kumbaka mtoto wake tayari ana kesi kama hizo nne za watoto wa wazazi wengine lakini hadi sasa hakuna hata kesi mmoja aliotiwa hatiani na yupo nje anaendelea na pirika zake kama kawaida.

 


‘’Nilikua na malengo makubwa na mtoto wangu nilimuandaa aje kuwa msomi bora huko mbeleni ili aweze kunisaidia lakini leo hii nimekua nikiona haya hata kutembea na nina wasiwasi watu wananicheka. ‘’aliongezea.


 

Mzazi mwengine aliwataka wazazi wenzake licha ya kuwepo kwa chanagmoto hizo kwa wazazi na walezi hawapaswi kukata tamaa kwani kukata tamaa ni kuhalalisha kuendelea kwa matendo hayo.


 

Alitole mfano kesi ya mtoto wake iliokua katika Mahakama ya Mwera ilikua haisikilizwi wala kuelezwa lolote lile lakini baada ya kuanza kutoa taarifa TAMWA-ZNZ maafisa wake walifuatilia na kesi yake kuanza upywa kusikilizwa na hivi karibu kesi hio itatolewa hukumu.

 

 

Hakimu wa Mahakama ya Mkoa Vuga  Valentina A.Katema alisema kesi zaudhalilishaji zina mlolongo mkubwa na kwamba mtu anaepaswa kuhukumiwa ni lazima atiwe hatiani bila kukosekana hata asilimia ndogo ya ushahidi.


 

Akizungumzia kuhusu suala la kutolewa kwa dhamana kwa watuhumiwa kwa kesi za udhalilishaji alisema dhamana hio hutolewa na Mahakama kuu kwa kuwa ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo kwa mujibu  wa sheria.


 

Akiendelea kufafanua zaidi alisema licha ya dhamana kwa matukio ya udhalilishaji kufungwa lakini Mahakama kuu ina uwezo wa kutoa  dhamama kwa kosa lolote ile kwa mujibu wa sharia hivyo inapotokea mtu hakuridhika na kupewa dhamana kwa mtuhumiwa anatakiwa kukata rufaa.


 

Akizungumzia kuhusu suala la ushahidi Mahamakani alisema hakuna kipengele chochote cha sharia  kinachozuia upande mmoja kutosikiliza ushahidi wa upande mwengine unapowasilishwa Mahakamani na kuwataka wahusika wanapotaka kuskiliza ushahidi wawasiliane na Mahakama na wataruhusiwa.


 

‘’Watu wanawajibu wa kufuatilia kesi zao na kuuliza Mahakama lini kesi yao itaendelea na iwapo kuna upande mwengine unatakiwa kutoa ushahidi basi hawazuiwi kuhudhuria.’’


 

Sambamba na hayo Hakimu huyo alizungumzia kuhusu madai ya rushwa kwa baadhi ya maafisa mbali mbali na kusema kuwa kwa sababu kwneye jamii kuna watu hawafahamu taratibu za kesi hico huona wanacheleweshwa na kutengezwa kwa mazingira ya rushwa.


 

Kwa upande wake Hakimu wa Mahakama ya Mwera Khamis Ali Simai alisema katika kesi ambazo zinawapa tabu kwenye ushahidi ni kesi za udhalilishaji hususani zile ambazo wahusika huanzia miaka 16 kuja chini.

 


Alisema kesi hizo ni ngumu sana kupata ushahidi wa kumtia mtu hatiani kwani wapo baadhi ya wazee huamua kuziharibu na kupteza ushahidi kwa sababu wanazozijua wao wenyewe.


 

Alisema iwapo Zanzibar inataka kuona mabadiliko makubwa ikiwemo kzuia matendo hayo yasitokee tena hakuna budi wazazi na walezi kuwa tayari kutoa mashirikiano na vyombo husika ili waliofanya matendo hayo wachukuliwe hatua kali mara moja.


 

Mkutano huo wa majadiliano ya siku moja umendeshwa na TAMWA-ZNZ na kushirikisha wadau 60 kutoka vyombo mbali mbali vya sharia na taasisi binafsi.


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.