Habari za Punde

Waumini wa Dini ya Kiislamu wataendelea kutekeleza wajibu wao wa kusimamisha Ibada kufuatia mafunzo waliyoyapata ndani ya Mafungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na Waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kukamilika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa hapo katika Msikiti wa Ijitimai ya zamani Magogoni Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi.

Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakifuatilia nasaha za Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla alip[ozungumza mara baada ya kumalizika kwa sala ya Ijumaa Magogoni.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Na.Othman Khamis.OMPR.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla alisema ni jambo la fahari na la msingi kama Waumini wa Dini ya Kiislamu wataendelea kutekeleza wajibu wao wa kusimamisha Ibada kufuatia mafunzo waliyoyapata ndani ya Mafungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan unaomalizika.

Mheshimiwa Hemed Suleiman aliyasema hayo wakati akisalimiana na Waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kukamilika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa hapo katika Msikiti wa Ijitimai ya zamani Magogoni Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi.

Alisema wajibu wa Waumini hao ni vyema ukalenga Zaidi katika mfumo wa mashirikiano, Umoja na Mshikamano utakaorahisisha matakwa waliyoyakusudia hatua mabayo kwa upande mwengine itaisaidia Serikali Kuu iliyojikita kwa dhati kuwahudumia Wananchi wake bila ya kujali itikadi za Kisiasa, Dini na hata maeneo.

Mheshimiwa Hemed Suleiman aliwaomba Waumin I na Wananchi hao kuendelea kuiamini Serikali yao iliyokusudia kuwaondolea kero na matatizo yanayowasumbua akiyataja baadhi yake kuwa ni pamoja na uhaba wa huduma za Maji safi kwa baadhi ya sehemu, Miundombinu ya Mawasiliano ya Bara  bara pamoja na ukali wa maisha kwa kuongeza fursa za Ajira kama zilivyoahidiwa wakati wa Kampeni za Uchaguzi.

Alisisitiza kwamba kile kinachokusanywa katika Mapato ya Serikali kupitia vianzio vyake tofauti kiwahudumie Wananchi wote na kamwe haitakuwa sahihi kuona baadhi ya Watu wachache wanaozingatia ulafi katika utekelezaji wa majukumu yao kwenye Taasisi wanazuhudumia Wananchi wanaendeleas kuachiwa kufanya uhalifu huo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alibainisha kwamba kuibuka kwa Wawekezaji wa Taasisi za Kigeni kuridhika na mazingira bora ya Rasilmali zilizopo Nchini ni mwanzo wa hatua za kuunga mkono Serikali Kuu katika Sekta ya Uwekezaji wa Mirtadi tofauti kupitia Rasilmali hizo.

Mheshimiwa Hemed Suleiman alifahamisha kwamba Maendeleo yote hayo yaliyoanza kuonyesha muelekeo mzuri ndani ya masuala ya Uwekezaji yataweza kufanikiwa vyema endapo suala la kudumishwa kwa Amani ya Nchi litazingatiwa na kupewa nafasi yake.

Mapema akitoa Hotuba ya sala ya Ijumaa Mwanazuonbi Sheikh Fadhil Moh’d Faki  alitanabahisha kwamba Waumini wanapaswa kuwa makini kwa kujiepusha na vitendo vya Shetani vinavyopelekea kutumbukia  katika matendo maovu.

Sheikh Fadhil Moh’d alisema Uislamu tayari umeshaelekeza njia sahihi za kumuepuka Shetani kwa kuziainisha ndani ya Aya za Kitabu Kitukufu cha Quran kilichomfafanua Shetani mwenye program maalum alizojiwekea za kumpoteza Muumini kama alivyochukuwa ahadi kwa Mwenyezi Mungu.

Aliwakumusha Waumini hao kwamba itapendeza wakizama Zaidi katika ucha Mungu hasa ndani ya kipindi hichi cha kumalizia kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wenye fadhila nyingi.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.