Na Fredy Mgunda,Iringa.
WANAFUNZI wa mkoa wa Iringa wanaoenda kushiriki mashindano ya UMISETA mwaka huu wamepewa kiasi cha shilingi laki moja na mkuu wa wilaya ya Iringa na wametakiwa kuhakikisha wanarudi na vikombe mbalimbali kutokana na michezo wanayoenda kucheza kwenye mashindano hayo.
Akizungumza wakati walipowatembelea wanafunzi hao walioweka kambi katika shule ya Sekondari ya Ifunda,mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa wamekaa kambini kwa muda ambao utawahakikishia kupata ushindi kwenye mashindano hayo.
Kasesela alisema kuwa wakishinda makombe kwenye mashindano hayo ya UMISETA watakuwa wameuwakilisha vizuri mkoa wa Iringa na watapewa zawadi kutokana na kazi waliyoifanya kwenye mashindano hayo.
Alisema kuwa ameamua kuwapatia kiasi cha shilingi laki moja kwa ajili ya kuwaongezea chachu ya kwenda kupambana kuhakikisha wanashinda michezo yote ambayo watakuwa wanashiriki kwenye mashindano hayo.
kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga alisema kuwa wanapaswa kuhakikisha wanaupigania mkoa wao kwa hali yoyote ile ili kuupatia heshima mkoa wa Iringa kwenye ngazi ya michezo kama ilivyokuwa miaka ya zamani.
Sendiga alisema wakifanikiwa kushinda makombe mbalimbali kwenye mashindano hayo watapokelewa kwa hadhi ya kitaifa kuanzia pale wanapoingia kwenye mipaka ya mkoa wa Iringa na kutakuwa na maandamano ya kupokea kwa ushindi huo.
Naye Mratibu wa safari hiyo Robert Luwanja alisema kuwa wanafunzi hao wamefanya mazoezi ya kutosha na wapo tayari kwa mapambano ya kuhakikisha wanaenda kushinda michezo yote wanayoshiriki kwenye mashindano hayo ya UMISETA mwaka huu.
Luwanja alisema kuwa msafara utakuwa na jumla ya watu 113 ambao ni wanafunzi pamoja na viongozi wanaenda kwenye mashindano ya UMISETA mwaka huu.
alisema kuwa anashukuru kwa kupata kambi bora ambayo walipata kila kitu amb acho walikuwa wanakihitaji kwa ajili ya maandalizi ya kwenye kwenye mshindano hayo na kutoa shukrani kwa mkuu wa wilaya ya Iringa kwa mchango wake ambao amekuwa anautoa na alioutoa wakati wa kuwaaga wanamichezo hao.
No comments:
Post a Comment