Habari za Punde

Timu ya KMKM Yaifikia Rikodi ya Timu ya Mlandege Kubeba Kombe la Ligi Kuu ya Zanzibar Mara 7

 

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar Timu ya KMKM Zanzibar wakishangilia Ubingwa wao baada ya kukabidhiwa Kombe wa Ubingwa kwa msimu wa mwaka 2021 /2022, kwa kuibuka Bingwa wa Ligi hiyo kwa kumaliza mchezo wao wa mwisho kwa ushindi uliofanyika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.

Timu ya KMKM SC imeweka rikodi sawa na Mlandege FC na kuwa Mabingwa wa Kihistoria kwenye Ligi Kuu Soka ya Zanzibar. 

Timu hizo (KMKM na Mlandege) ndio wanaongoza kubeba Ligi kuu soka ya Zanzibar mara nyingi (7) wakifuatiwa na Small Simba kushika nafasi ya 3 kwa kutwaa kombe hilo mara 5.

KMKM Walibeba (7)
1984
1986
2004
2012-2013
2013-2014
2018-2019
2020-2021

Mlandege Walitwaa (7)
1996
1997
1998
1999
2001
2002
2019-2020

Small Simba Walishinda (5)
1983
1985
1988
1991
1995

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.