Habari za Punde

Wananchi Mkoani Tanga Waitwa Nssf, Waajiri Wasiochangia Mfuko Kuburuzwa Mahakamani.

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

Baada ya mabadiliko ya sheria iliyofanyoka katika Mifuko hiyo mwaka 2018 Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (Nssf) umebeba kundi kubwa la Watanzania hivyo wanatumia fursa ya kushiriki kwenye maonyesho mbalimbali ya Kitaifa ili kuhahakikisha wanatoa elimu kwa umma.

Hayo yalisemwa jana na Meneja Uhusiano  na Elimu kwa Umma Nssf makao makuu Lulu Mengele katika ufunguzi wa maonyesho ya wiki ya maziwa yaliyofanyika viwanja vya Tangamano jijini Tanga na kusema lengo ni kuendelea kutoa elimu katika sekta binafsi na sekta ambazo siyo rasmi.

"Kwahiyo tumeona tuje kwenye maonyesho hayao haya kuna wadau mbalimbali ambao Nssf tunafanya nao kazi moja kwa moja na tumeona tutumie fursa kuwapa elimu wadau wetu kwa upande wa  sekta binafsi nà sekta zisizo rasmi' alisema.

Mengele alibainisha kwamba kuna kero mbalimbali ambazo wanachama wao wanazipata kupitia mfuko ambapo ili kuwafikia na kuwasaidia kuzitatua wanapaswa kufika kwenye maonyesho kama hayo laliki pia kuwapa elimu wanancho wengine ambao ambao hawajajiandikisha.

"Nipende kuwaambia wananchi wote wa mkoa huu wa Tanga waweze kufika katika banda letu ili waweze kupata elimu na vilevile waweze kujiunga na mfuko huu na kupata fursa ya kupata huduma zetu zinazotolewa na mfuko huu wa hifadhi za jamii" aliongeza Mengele.

Sambamba na hayo Mengele alieleza kwamba wameona watoe elimu kwa wanafunzi waliofika eneo hilo ili kuwajenga kifikra kuelewa maana ya hifadhi kutokana na walio wengi kuona mifuko hiyo haifai na inafanya kazi ya kukusanya fedha za watu nila mafanikio kwa wahusika huku wakiamini elimu hiyo itawasaidia watoto hao kuwa mabalozi wazuri katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

"Tumeona pia leo tuwape elimu hawa wanafunzi kwakuwa hawa ndio viongozi wa kesho, hili ndilo Taifa la kesho, hivyo tumeona tuwapatie elimu nyepesi ili wanapokua wanaelewa nini maana ya mfuko wa hifadhi ya jamii, kwasababu ukiweza kujua nini maana ya hifadhi mapema baadae inakua rahisi kujihifadhia fedha" alisisitiza.

"Kuna msemo unaosema, samaki mkunje anali mbichi kwahiyo ukimpa elimu akiwa mdogo ataenda kuwa balozi mzuri na hatotamani kuchukua hela yake na kuitumia kwakua atakua anajua maana ya kuhifadhi" aliongeza.

Naye Ofisa Mwandamizi Idara ya Matekelezo mkoa wa Nssf Tanga Aboubakar Sudi alisema kupitia maonyesho hayo wanatekeleza agizo la serikali la kuwafikia sekta zisizo rasmi na wafanyabiashara wadogo wadogo baada ya mabadiliko ya sheria ili kufikiàlengo la kuwafikia wananchi milioni kumi na nane.

"Katika kutekeleza maagizo yale na kupinguza umasikini kwa wananchi na kuongeza wigo wa uandikishaji, Nssf tumeona tushiriki kwenye maonyesho haya na dhumuni kubwa ni kuwahudumia wafanyakazi wa sekta zisizokuwa rasmi na wananchi, hivyo tutakuwa hapa kwa wiki nzima ili kuwaonyesha bidhaa tulikuwanazo, mafao na huduma za Nssf, taratibu za wanachama ama kupata mafao yake" alisema.

Sudi alibainisha kwamba kwa upande wa waajiri watakaoshindwa kuchangia mfuko wa Nssf mkoani hapa kwa mwaka wa fedha unaoishia mwezi juni mwaka huu  wako mbioni kuchukuliwa hatua za kisheria na kupelekwa mahakamani.

Aidha alifafanua kwamba kwa mkoa wa Tanga waajiri wanaochangia hawachangii kwa wakati lakini pia wapo ambao hawachangii kabisa  hivyo, wameshirikiana na Ofisi ya mkuu wa mkoa na Taasisi nyingine wanazofanya nazo kazi wamekuwa na ziara za kushtukiza na sasa kuelekea mwaka wa fedha kwa Nssf walikua na zoezi la kuorodhesha majina ya waajiri wote ambao hawana mwamko wa kulipa au kulipa kwa wakati.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.