Habari za Punde

KIKOSI MAALUM CHA KUZUIYA MAGENDO (KMKM) CHASHEREHEKEA MIAKA 48 TOKEA KUBADILISHWA JINA KUTOKA JINA LA NEVY.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa akiwa kwenye sehemu maalum akipokea salamu za Bendera katika Sherehe za KMKM DAY zilizofanyika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
 Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana Mustafa akiwa na kiongozi wa gwaride Luteni. Mary Maico Hafidhi akipita kukagua gwaride lililoandaliwa katika madhimisho ya KMKM DAY.
Kikundi cha gwaride gadi ya wanawake kikipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana kutoa heshima.
Timu ya kuvuta Kamba ya Nyuki (JWTZ) wanaume (kushoto) na timu ya KMKM wakishindana kuvuta kamba ambapo timu ya kmkm imewavuta timu pinzani.
 Mkuu wa KMKM Commodore Azana Hassan Msingiri akiwakabidhi Cheti cha Shukrani kwa Mkuu wa Mo Dewji Foundation Ms Rachel Carp (alievaa miwani) akiwa na mwenzake kwa mchango wao walioutoa kufanikisha sherehe za KMKM DAY.
Kepteni wa Timu ya Mpira wa Miguu ya KMKM SC Makame Haji Mngwali akionyesha Kombe la ubingwa wa KMKM DAY waliloshinda dhidi ya timu ya KVZ baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana Mustafa katika Madhimisho ya kmkm day yaliyofanyika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa akiwahutubia katika sherehe za KMKM DAY zilizofanyika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.

Baadhi ya viongozi wakuu wakifuatilia hutuba ya Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana (hayupo pichani) katika Kilele cha KMKM DAY.

Picha na Makame Mshenga KMKM.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.