Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Mpango Ahudhuria Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa Paris Nchini Ufaransa.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru kenyatta mara baada ya kuwasili katika  ukumbi wa Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum) Paris Nchini Ufaransa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akifuatilia Mada mbali mbali zinazowasilishwa katika Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum) Paris – Ufaransa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akifuatilia Mada mbali mbali zinazowasilishwa katika Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum) Paris – Ufaransa.

Na.OMR -Ufaransa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amehudhuria ufunguzi wa Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa (Generation Equality Forum) linalofanyika Paris Nchini Ufaransa. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Jukwaa hilo.

Jukwaa hilo lenye madhumuni ya kuchagiza Usawa wa kijinsia linajadili Umuhimu wa uwezeshaji wanawake kiuchumi kama nyenzo ya kumnyanyua mwanamke kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

 Kati ya mambo yaliyojadiliwa katika jukwaa hilo ni kumwezesha mwanamke kupata Teknolojia rahisi na sahihi katika kufanya shughuli za kiuchumi; kutolewa mafunzo ya ujasiriamali pamoja na utoaji wa mitaji kwa wanawake pamoja uwepo wa mifumo sahihi ya kidigitali katika shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wanawake.

Katika Jukwaa hilo hii leo Julai 1,2021 Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango anatarajia kutoa Ahadi za Tanzania kama kinara wa uwezeshaji wanawake kiuchumi kama ilivyoridhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.