Mbunge wa Nanyamba Mhe. Abdallah Chikota akizungumza katika kikao cha
ndani katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara wakati Naibu Waziri wa
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (katikati) alipotembelea
Wilaya hiyo ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu katika Mkoa wa
Mtwara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, ujenzi,
uwezo na ubora wa minara ya mawasiliano, mwingiliano wa mawasiliano mipakani na
usikivu wa redio ya Taifa TBC.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan
Kyobya.
Mbunge wa Lulindi Mhe. Issa Mchungaela akizungumza katika kikao cha ndani katika
ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara wakati Naibu Waziri wa Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew alipotembelea Wilaya hiyo ikiwa
ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu katika Mkoa wa Mtwara ya kukagua maendeleo
ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, ujenzi, uwezo na ubora wa minara
ya mawasiliano, mwingiliano wa mawasiliano mipakani na usikivu wa redio ya
Taifa TBC.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo
Mathew akizungumza katika kikao cha ndani katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Mtwara kabla ya kuanza ziara yake wilayani humo ambapo alitembelea bandari ya
Mtwara kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya simu na Mkongo wa Taifa
wa Mawasiliano uliofikishwa bandarini hapo pamoja na kutembelea baadhi ya
maeneo yenye changamoto ya mawasiliano ya simu katika kata ya Mitengo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (wa pili kushoto) akimsikiliza Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara Nobert Kalimbu (kushoto) wengine kutoka kulia ni Mbunge wa Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya wakati wa kukagua ufikishaji wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano bandarini hapo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo
Mathew (wa tatu kulia) alipotembelea bandari ya Mtwara kwa lengo la kukagua
miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano uliofikishwa katika bandari hiyo
kwa lengo la kuwezesha mawasiliano ya simu na intaneti yenye kasi kubwa na
uwezo mkubwa Kulia ni Mbunge wa Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga akifuatiwa na
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya. Wengine ni wafanyakazi wa bandari
na baadhi wataalam aliombatana nao katika ziara hiyo
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo
Mathew akikagua na kutoa maelezo kuhusu Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa
Mbunge wa Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga alipozuru katika bandari ya Mtwara tarehe
11.7.2021 ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu katika Mkoa huo ya
kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, ujenzi, uwezo na
ubora wa minara ya mawasiliano, mwingiliano wa mawasiliano mipakani na usikivu
wa redio ya Taifa TBC.
Na Mwandishi wetu, MTWARA
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew amefanya ziara ya kukagua ufikishaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika bandari ya Mtwara uliofanywa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), upatikanaji wa mawasiliano ya simu katika eneo hilo pamoja na mifumo ya TEHAMA inayotumika bandarini hapo
Katika ziara hiyo Mhe. Mhandisi Kundo ameambatana na wataalam kutoka taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo ambazo ni Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Shirika la Posta Tanzania (TPC) pamoja na wenyeji wake ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini Mhe. Dunstan Kyobya na wabunge wa majimbo matatu yaliyopo katika Mkoa wa Mtwara ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu katika Mkoa wa Mtwara ya kukagua ubora na upatikanaji wa huduma za mawasiliano, Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, mwingiliano wa mawasiliano mipakani na usikivu wa radio ya Taifa TBC
“Nimefika hapa kujiridhisha uwepo wa nyaya za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika bandari ya Mtwara zitakazofanikisha upatikanaji wa intaneti yenye uwezo mkubwa na kasi kubwa ili shughuli zote zinazoendelea bandarini zisikwame kwasababu ya kukosekana kwa huduma ya intaneti” alizungumza Mhandisi Kundo
Aidha, pamoja na kukagua ufikishaji wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa katika bandari hiyo pia alitumia muda huo kukagua mifumo ya TEHAMA inayotumika kwenye bandari hiyo kama inafanya kazi na kusomana na kutoruhusu mianya ya upotevu wa mapato na kukagua upatikanaji wa mawasiliano ya simu katika eneo la bandari hiyo
Katika hatua nyingine Mhe. Mhandisi Kundo alizungumzia mwingiliano wa mawasiliano ya simu na nchi jirani ya Msumbiji yaliyolalamikiwa na wabunge na kutolea ufafanuzi kuwa mwingiliano wa mawasiliano katika maeneo ya mipakani yanasababishwa na uwezo wa minara ya mawasiliano iliyopo eneo husika pamoja na ramani ya mipaka ya kijiografia ya eneo husika inavyoingia na kutoka hivyo kusababisha eneo lenye mtandao wenye nguvu zaidi ndio utakaopatikana
Aliongeza kuwa Wizara hiyo ipo katika hatua za kuhakikisha minara inayojengwa kuanzia sasa inakuwa na uwezo wa 3G na kuendelea pamoja na kuiboresha minara ya zamani iliyokuwa na uwezo wa 2G kwenda 3G na kuendelea ili kuhakikisha kunakuwa na mitandao yenye nguvu itakayowezesha kupatikana kwa huduma ya mawasiliano ya simu na intaneti
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wabunge wa majimbo matatu ya Mtwara Mjini Mhe. Abdallah Chikota (Mb) Nanyamba, Mhe. Hassan Mtenga (Mb) Mtwara Mjini na Mhe. Issa Mchungaela (Mb) Lulindi, mbali na kuzungumzia mahitaji ya huduma za mawasiliano katika maeneo yao kwa niaba ya wananchi pia walitumia fursa hiyo kumshukuru Mhandisi Kundo kwa kufanya ziara hiyo na kuahidi kuendelea kushirikiana ili kutatua changamoto za mawasiliano zilizopo katika Mkoa huo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
No comments:
Post a Comment