Habari za Punde

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda ziarani Pemba kujionea changamoto za ununuzi wa karafuu

WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaabani (kulia), akiangalia karafuu gredi ya kwanza zilizohifadhiwa ndani ya kopo, katika kituo cha ununuzi wa karafuu Madungu Chake Chake, wakati wa ziara yake ya kuangalia changamoto za ununuzi wa karafuu kutoka kwa wakulima baada ya shirika kuingia katika mfummo mpya wa malipo ya Kidigitali.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban, akisikiliza changamoto kutoka kwa mmoja ya wachukuzi wa kituo cha ununuzi wa karafuu Madungu Chake Chake, wakati wa ziara yake ya kuangalia changamoto za ununuzi wa karafuu kutoka kwa wakulima baada ya shirika kuingia katika mfumo mpya wa malipo ya Kidigitali.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban, akizungumza na wakulima wa zao la Karafuu katika kituo cha ununuzi wa zao hilo Madungu Chake Chake, baada ya kusikiliza changammoto zao, kufuatia shirika kuingia katika mfumo mpya wa malipo ya Kidigitali.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban, akiangalia karafuu kavu kutoka kwa mkulima wa zao hilo Pemba Mwanahawa Fadhil Mohamed, wakati wa ziara yake ya kuangalia changamoto za ununuzi wa karafuu kutoka kwa wakulima baada ya shirika kuingia katika mfumo mpya wa malipo ya Kidigitali.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.