Habari za Punde

Ziara Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Magharibi Mhe Tauhida


 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Magharibi Mhe Tauhida Gallos Nyimbo amewasisitiza madakari na wauguzi wa kituo cha Afya cha Fuoni kuendelea kufanya kazi kwa moyo wa kizalendo katika kuwahudumia wananchi ili kuweza kuondoa malalamiko yao kuhusu kile wanachokiita  utoaji mbovu wa huduma hasa katika vituo vya serikali.

 Mhe Tauhida ametoa ushauri huo wakati alipotembelea kituo cha Afya Fuoni Kwa Ajili Ya Kuwakagua Wagonjwa Pamoja Na Kujionea Utaratibu Wa Huduma Zinavyotolewa Kituoni Hapo.

Ameeleza kuridhishwa na utaratibu mzuri waliojipangia wafanyakazi wa kituo hicho pamoja na kuweka mbele uzalendo wa taifa katika kuwahudumia wananchi bila ya kujali tofauti za dini, rangi, jinsia wala kabila.

 Amefahamisha kuwa mapenzi yao kwa wagonjwa katika kuwahudumia ndio sababu inayopelekea kituo hicho kupata sifa kubwa na kuwa kimbilio la wagonjwa kutoka maeneo mbali mbali ya Zanzibar.

 Mapema Mhe Tauhida alikabidhi baadhi ya vifaa muhimu katika kituo hicho ikiwemo sabuni za usafi, viti vya wagonjwa  na taula za wanawake ambapo msaidizi muuguzi katika kituo hicho dkt abdallah twaha issa alimshukuru mbunge huyo kwa ziara yake hiyo pamoja na kukabidhi vitu ambavyo vitaweza kuwasaidia waginjwa pamoja wafanyakazi katika shughuli zao za kila siku.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.