Habari za Punde

Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Viungo Visiwani Zanzibar Ukiendelea Kwa Kasi Eneo la Darajani

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa Serikali za mitaa na idara maalumu za SMZ Mhe. Massoud Ali  Mohamed akisistiza jambo wakati alipotembelea ujenzi wa jengo hilo Darajani mjini Unguja.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa Serikali za mitaa na idara maalumu za SMZ  Massoud Ali  Mohamed akitoa maelezo ya mbele ya waandishi w ahabari kuonesha kuridhishwa kwake na ujenzi wa jengo hilo.
Meneja Mkuu  utekelezaji mradi wa Viungo Zanzibar Amina Ussi Khamis akitoa maelezo kuhusu lengo la ujenzo wa jingo hilo kwa waandishi wa habari.
Muonekano wa baadhi ya sehemu ya ujenzi wa jengo hilo unavyoendelea hadi sasa ambapo umefikia kwa asilimia 60 na unatarajiwa kukamilika mnamo mwezi oktoba mwaka huu.

Na Muhammed Khamis

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa Serikali za mitaa na idara maalumu za SMZ Mhe. Massoud Ali  Mohamed amesema utekelezaji wa mradi wa viungo visiwani Zanzibar unachangia  kasi ya maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa wananchi wake hususani kupitia sekta ya kilimo.

 

Waziri Massoud aliyasema hayo alipotembelea ujenzi wa jengo maalumu litakalotumika kama sehemu ya kuhifadhia bidhaa za matunda na mboga mboa bila ya kuharibika (Jokofu) pamoja na sehemu ya kufanya biashara za bidhaa hizo katika eneo la Darajani mjini Unguja.

 

Alisema wao kama Serikali wamefarijika kwa kiasi kikubwa juu ya uwepo wa mradi huo na kwamba unasaidia kutekeleza ahadi za Serikali kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wakulima kulima kilimo cha kisasa sambama na kuongeza idadi ya ajira.

 

Pia Waziri huyo alieleza kuwa kwa kuwa soko la darajani ni moja ya masoko ya kale Zanzibar hivyo kujengwa kwa jingo hilo jipya kutaacha alama sambamba na kuifanya haiba ya maeneo hayo yenye kuvutia kwa wenyeji na wageni wanaotembeela kila leo visiwani hapa.

 

Katika hatua nyengine  aliwataka watendaji wa mradi huo kwa kushirikiana na Baraza la Manispaa kuhakikisha wanawarudisha wafanya biashara wote walioondolewa katika eneo hilo ambalo linatumika kwa ajili ya ujenz huo na sio kufanya vyenginevyo pindi ujenzi wa jesho hilo utakapokamilika.

 

Akiendelea kufafanua zaidi Waziri Massoud  alisema haitapendeza na nikinyume na utaratibu kuona mtu yoyote yule anatumia nafasi yake kuhodhi nafasi katika jingo hilo na kuwapa watu wake au yeye mwenyewe na kwamba watakaobaika kufanya hivyo watachukuliwa hatua zinazotahiki dhidi yao.

 

Akitoa ufafanuzi kuhusu lengo la ujenzi wa jingo hilo Meneja mkuu wa utekelezaji wa mradi huo Amina Ussi Khamis alisema mradi uliamua kujenga jingo hilo kwa lengo la kunusuru kuharibika kwa mazao mengi ya wakulima visiwani hapa kutokana na kushindwa kuwepo kwa sehemu maalumu ya kuhifadhia bidhaa hizo.

 

Pia alisema kuwepo kwa jengo hilo jipya katika ameneo ya karibu na bandari kutawawezesha wakulima na wafanya biashara kusafirisha bidhaa zao nje ya Zanzibar zikiwa bado ni salama bila ya kuharibika na kwamba watakua na uhakika wakujingizia kipato kupitia bidhaa zao.

 

Aidha alisema kabla ya ujenzi huo eneo hilo lilikua likitumiwa na wafanya biashara wa mboga mboga na matunda wapatao 33 na watahakikisha ndio watakua wa kwanza kurudi kwenye jingo hilo pindi litakapokamilika na sio watu wengine ambao hawakua miongoni mwa wafanya biashara wa eneo hilo.

 

Akitoa ufafanuzi kuhusu sehemu maalumu ya kuhifadhia mboga mboga na matunda bila ya kuharibika (jokofu)alisema jengo hilo litakua na sehemu maalumu ambayo itakua na uwezo wa kuhifadhi wastani wa tani 7 hadi 13 za bidhaa hizo.

 

Akieleza kuhusu gharama za ujenzi huo alisema ujenzi huo utagharimu   milioni 342 za kitanzania hadi kukamilika kwake  na unasimamiwa na kampuni ya White Pelican Limited chini ya usimamizi mkandarasi wa ushauri kutoka kutoka kampuni ya ZANPLAN LMITED na hadi kufikia sasa mradi huo umetekelezwa kwa asilimia 6O.

 

Mradi wa utekelezaji mradi wa viungo visiwani hapa unatekelezwa na PDF,TAMWA-ZNZ pamoja na CFP Chini ya ufadhili wa umoja wa ulaya (EU) na utatekelezwa kwa muda wa miaka mine huku ukilenga wanufaika wapatao 57,000 kutoka katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.