Habari za Punde

Ujio wa Viongozi wa Mpira wa Miguu Kutoka Nchini Egypt Kutoa Fursa Soka la Zanzibar

Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid akizungumza na CEO wa Kampuni ya Captex kutoka Nchini Egypt Bw.Mohamed Hassan Abouzeid, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo Migombani Jijini Zanzibar.akiwa na Mwenyekiti wa ZFF 

Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid amesema ujio wa viongozi wa mpira wa miguu kutoka Egypt umeahidi kuekeza Zanzibar katika michezo ili kuwapatia fursa na kunyanyua soka nchini.

Akizungumza na ugeni huo baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo huko Migombani Mjini Unguja.

Alisema ujio huo utafungua milango na fursa za michezo kwa vijana pamoja na fursa nyengine za kuekeza katika utalii kwa kisiwa cha Unguja na Pemba  ili kuongezeka kwa wageni .
Mhe.Tabia alieleza wameahidi kurejesha utamaduni uliopo zamani kwa timu ya Taifa ya Zanzibar kwa kukaaa kambi nchini Egypt kwa lengo la kupata uzoefu na mazoezi zaidi.

“ Viongozi wa mpira wa miguu  kutoka Egypt wametuahidi mambo mengi ya kutuletea maendeleo nchini kwetu  tumefarajika kama Wizara lakini pia serikali yetu ya awamu ya nane imetilia mkazo masula ya michezo ,uwekezaji na kukuza utalii “ alisema

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na  kudumisha  mahusiano na Serikali ya nchini  Egypt kwa kutekeleza ilani na kumsaidia Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi  katika kukuza mahusiano na nchi jirani.

Nae CEO kutoka Kampuni ya Captex kutoka Egypt Mohamed Hassan Abouzeid alisema wapo teyari kuendelea kushirikiana na Zanzibar katika kuimarisha na kukuza  michezo ,pamoja na kuekeza ili kuona mpira wa  miguu Zanzibar unapiga hatua.

Aidha Serikali ya Egypt imeahidi pia kutoa vifaa vya michezo na  uekezaji na kuekeza sehemu nyengine za utalii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.