Habari za Punde

Viongozi,watumishi wa Umma Mfano wa Kuigwa Kujali Afya.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa akizungumza na menejimenti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Na.Adeladius Makwega .WHUSM-Dodoma

Serikali imesema kuwa viongozi na watumishi wa umma wana wajibu wa kutilia maanani masuala ya afya hata kama baadhi ya mambo haya ni ya hiari. Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo mheshimiwa Innocent Bashungwa wakati akizungumza na menejimenti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

 

“Kuna masuala ya ugonjwa  wa UKIMWI huu ni ugonjwa hatari sana kwa afya zetu na afya za familia zetu kwani kama sisi kama wakuu wa wafamilia tusipokuwa makini tunaweza kuziangamiza na kuangamiza familia ni kuangamiza taifa.”Alisema kwa Mhesmiwa Bashungwa.

Ni kweli mimi kama Waziri ninakwenda kusoma mkakati wa ugonjwa  Fulani Bungeni lakini vipi hali hii ilivyo katika Wizara yangu? Aliuliza. Siyo jambo jema kama watumishi na menejimenti yangu ikaathirika na ugonjwa huo.

 

“Ninampongeza Msemaji wa Serikali na Mkurugeniz wa Idara ya Habari Maelezo ndugu  Gerson Msigwa kwani amekuwa akinikumbusha juu ya suala hili la UVIKO 19 maana nilichanjwa mapema kabisa na kule jimboni waliniuliza vipi mheshimiwa umeshachanjwa nikawaijibu ndiyo na nikawaonesha na picha na hilo pia linawahamasisha wananchi kuchanjwa.”Alisema mheshimiwa Bashungwa.

 

Aliongeza kuwa athari za Korona zipo na watu wanapoteza maisha yao, kila siku ninapata taarifa kutoka jimboni kuwa mtu fulani amefariki, jamani Korana ipo.

Wizara tuna jukumu la kuelimisha umma kwa kutumia vyombo vyetu, na idara zetu za Sanaa na Utamaduni kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali.

 

“Vyombo hivi ni silaha kubwa sana katika kupambana na magonjwa haya japokuwa suala la magonjwa linashirikisha wizara zingine. Nawaambieni hivi ni vita na ili kuvishinda lazima kutumia kila silaha tuliyonayo ili tushinde.” Aliendelea kusisitiza.

 

Akizungumza mara baada ya maagizo hayo Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa wizara hii ndugu Petro Lyatuu amesema kuwa vyombo vyote vilivyo chini ya wizara vilianza kutekeleza majukumu haya ya kutoa elimu kwa umma lakini sasa vinapaswa kuongeza nguvu zaidi kutokana na maagizo ya Waziri Bashungwa.

 

“TBC na TSN wana kazi mbalimbali zinazofanywa juu ya magonjwa haya kama vile makala, habari na matangazo tuna hakika wasanii wetu wameshatunga nyimbo zenye maudhui ya Korana kama vile wimbo waaah wa msanii Diamond.” Tutaongeza juhudizadi aliongeza Kiongozi huyo wa Idara ya Sera na Mipango.

 

Wakizungumza mara baada ya kukamilika kikao hicho watumishi wa wizara hiyo wamesema kuwa ni kweli sasa kila mmoja wao anajua umuhimu wa kutunza afya zao kwani  kumekuwepo na jitahada za uvaaji wa barakoa na kuwekwa viminika vya kunawia mikono na tahadhari za UKIMWI wizarani hapo.

 

“Afya ni jambo la msingi unapoleta ubishi unaweza kwenda na maji, tunapaswa kupambana na magonjwa haya kwa juhudi zetu zote.” Alisema Francis Songoro ambaye ni Afisa Utamaduni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.