Habari za Punde

ZAWA yashauriwa kuweka mita kwenye mahoteli na viwanda ili kuongeza ukusanyaji wa mapato


Mwenyekiti wa kamati ya kuchunguza na kudhibiti hesabu  za serikali  za mitaa  na mashirika (laac) Habibu Ali Mohammed

 

Na Mwandishi wetu 


Kamatı ya Kuchunguza na kudhibiti hesabu  za serikali  za mitaa  na mashirika (laac) imeishauri mamlaka ya maji zanzibar ZAWA kuhakikisha wanapanga mipango mizuri ya kuweka mita katika mahoteli na viwanda ambavyo bado havijafungwa mita hizo ili kuweza kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya fedha za umma.

 

Ushauri huo wameutoa wajumbe wa kamati hiyo chini ya mwenyekiti wake mhe Habibu Ali Mohammed wakati walipokua wakipokea majibu ya  hoja za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali zilizojitokeza katika mwaka 2019/2020 .

 

Wamesema hoteli na viwanda ndio wateja wakubwa na ndizo sehem ambazo zinatumia maji kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na maeneo mengine ambapo ikiwa kutakua na mita kutaweza kuisaidia mamlaka kukusanya mapato zaidi ya kuweza kuendesha na kutekeleza mipango yake ya maendeleo.

 

Aidha wameishauri mamlaka hiyo kujipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanapata maji kwa wakati pamoja na kuwa na mikakati mizuri ya ukusanyaji ili serikali iweze kupata mapato.

 

Mkurugenzi mkuu wa mamalaka ya maji zanzibar zawa dkt salha mohammed kassim ameihakikishia kamati hiyo kuwa kwa sasa wamejipanga vyema kuhakikisha maeneo yote yatapata maji ndani ya kipindi kifupi kijacho ili kuweza kuongeza idadi ya wateja wapya watakaosaidia kuongeza mapato ya serikali kupitia sekta ya maji.

 

Kuhusu kutofikia malengo katika matumizi na mapato  kwa mwaka 2019/2020 dkt salha amefahamisha kuwa kuwepo kwa ugonjwa wa virusi vya  uviko 19 kumepelekea kupoteza wateja wengi wakubwa wa mamlaka kwa kufunga biashara zao pamoja na watumiaji wengi kukwepa kulipia huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.