Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi azindua boti za wananchi wa visiwa vya Makoongwe na Kisiwapanza Mkoani Pemba

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizindua Boti za Wananchi wa Visiwa vya Makoongwe na Kisiwapanza kwa ajili ya usafiri kutoka katika visiwa hivyo, uzinduzi huo umefanyika katika Bandari ya Mkoani Pemba, na (kulia kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Operesheni Kamanda wa KMKM CDR.Hussein Ali na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Mattar Zahor Masoud.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Operesheni Kamanda wa Kikosi cha KMKM CDR.Hussein Ali, akitowa maelezo ya kitaalamu ya Boti za Wananchi wa Visiwa vya Makoongwe na Kisiwapanza kwa ajili ya kuvukia, hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika katika Bandari ya Mkoani Pemba leo 3-9-2021.
WANANCHI wa Wilaya ya Mkoani Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Wananchi hao baada ya kuwazindua Boti za Wananchi wa Visiwa vya Makoongwe na Kisiwapanza kwa ajili ya usafiri wa kuvukia sehemu ya pili, hafla hiyo imefanyika katika Bandari ya Mkoani Pemba leo 3-9-2021
MWANANCHI wa Mkoani Pemba Bw. Mohammed Gulam akizungumza na kutowa kero yake, wakati wa mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) na Wananchi wa Waliya ya Mkoani uliofanyika katika viwanja vya Bandari ya Mkoani.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisoma barua ya Mwananchi wa Wilaya ya Mkoani, baada ya kuwasilisha kero zake, wakati wa mkutano huo wa kuwasikiliza Wananchi uliofanyika katika viwanja vya Bandari ya Mkoani Pemba na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.Mhe.Mattar Zahor Masoud.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Mkoani Pemba,baada ya kusikiliza kero zao akiwa katika ziara katika Mkoa wa Kusini Pemba, mkutano huo umefanyika katika viwanja vya Bandari ya Mkoani.
(Picha na Ikulu)  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.