Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe Tony Blair Ikulu Zanzibar.yiV

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe Tony Blair, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika leo 30-9-2021, katika ukumbi wa Ikulu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, leo Septemba 30, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe. Tony Charles Blair, Ikulu Zanzibar.

Mhe. Rais Dk. Mwinyi amemshukuru Mhe. Blair kwa ujio wake wa mara ya pili visiwani Zanzibar katika muendelezo wa ushirikiano baina ya Taasisi ya Mabadiliko Ulimwenguni ya (Tony Blair Institute For Global Change) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi amesema taasisi hiyo itakuwa na jukumu la kuisadia Serikali katika kubadilisha mifumo na kuhakikisha sera na mipango ya Serikali ya Awamu ya Nane inafanyika kwa vitendo, Uwezeshaji kiuchumi pamoja na kuwajengea uwezo watendaji wa Serikalini.

Rais Dk. Mwinyi ameongeza kuwa maeneo muhimu ambayo taasisi ya Tony Blair itawekeza nguvu ni pamoja na Sekta za Uchumi wa Buluu ikiwemo Utalii, Mafuta na Gesi baharini, Bandari na Uvuvi. Aidha Wataalamu wa taasisi hiyo wataisaidia Serikali katika Sekta za Kijamii ikiwemo Elimu, Maji, Barabara, Umeme na Uwezeshaji wa Ajira kwa Jamii.

“Hatuna shaka kupitia uzoefu wake tutaweza kufanikiwa ikiwa tutafuata miongozo na maelekezo ya wataalam wao watakavyotuelekeza”. Alisema Rais Dk. Mwinyi.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza. Mhe. Tony Blair amesema, Taasisi yake imefurahishwa na kuridhishwa na kazi inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Nane chini ya Rais Dk. Mwinyi na iko tayari kushirikiana na Serikali katika kuboresha mifumo na kujenga taasisi imara.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Waziri Mkuu Mstaaf wa Uingereza Mhe.Tony Blair, mazungumzo hayo yamefanyika  katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar
WAZIRI Mkuu Mstaaf wa Uingereza Mhe. Tony Blair akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali (hawapo pichani) baada ya kumaliza mazungumzo yake na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair (kushoto kwake) yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongozana na mgeni wake Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair,baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.