Na.Raya Hamad.– OMKR
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar D. Shajak ameitaka Tume ya UKIMWI Zanzibar kukabiliana vyema na mazingira ya sasa kwa kutumia mbinu na kuibua mawazo mapya ambayo yatazidisha mapambano dhidi ya maambukizi ya UKIMWI
Dkt Shajak
ameyasema hayo alipofanya mazungumzo na viongozi pamoja na watendaji wa Tume ya
UKIMWI ambapo amesisitiza kuwa jitihada zinazofanyika sasa katika kukabiliana
na maambukizi ya UKIMWI yaende mbali zaidi kwa vile dunia hivi sasa nguvu kubwa
imewekezwa kwenye kupambana na virusi vya Korona
Amesema
ugonjwa wa Korona umeipelekea jamii kujisahau kama ugonjwa wa UKIMWI bado upo hivyo
Tume ya UKIMWI iendelee kuchukuwa nafasi yake katika kuelimisha jamii na
kuhakikisha hakuna maambukizi mapya ya VIRUSI vya UKIMWI ifikapo 2025
“juhudi
zetu zilenge mafanikio na kufikiria njia mbadala za kutatua matatizo yaliyopo,
mpango mkakati wa nne ni vyema sasa ukaangalia mawazo mapya yatakayotuvusha
hapa tulipo ili tuondokane na maradhi ya UKIMWI” alisisitiza
Nakueleza
kuwa lengo la kupunguza na kuondokana na idadi ya maambukizi ya virusi vya
UKIMWI kutoka kawa mama kwenda kwa mtoto linafikiwa, Vijana na makundi maalum
kufikiwa katika kupewa elimu, wenye mahitaji kupatiwa dawa na tiba sahihi
Nae
Mkurugenzi mtendaji Tume ya UKIMWI Dkt Ahmeid M. Khatib amemuelezea Katibu Mkuu
kuwa katika kufikia malengo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Tume inawajibu wa
kutayarisha mkakati maalum na wadau wote wanajukumu la kuufuata mkakati huo
Tume ya
UKIMWI inaendelea na matayarisho ya Mkakati wa nne wa UKIMWI utaogusa sekta
zote kama taasisi za Serikali ama binafsi pamoja na jamii kwa vile wadau wote
ni wa mapambano ya UKIMWI na hivyo ni wajibu wa kila anaeguzwa kuhakikisha
malengo ya nchi na dunia yanafikiwa
Amesema mafanikio
yaliyopatikana katika kudhibiti maradhi ya UKIMWI yamepelekea Zanzibar kufikia chini
ya asilimia moja ya kiwango cha maambukizi ambapo nchi chache zimeweza kufikia
malengo haya na kuifanya Zanzibar iwe ni moja kati ya nchi zenye mafaniko
Dkt Ahmeid
amesema hadi kufikia mwaka 2020 malengo na shabaha za dunia ni kuhakikisha kuna
90 tatu ambazo zinafikiwa, na Zanzibar imefanikiwa kufikia asilimia 90 na amehakikisha
asilimia 90 ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI wanaojitambuwa ni asilimia
94, wanaojitambua na wanaotumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI
ni asilimia 98 na wanaotumia dawa ambao wameweza kuvishusha virusi ndani ya
mwili ni asilimia 93
Wakitoa
maoni yao wafanyakazi wa Tume ya UKIMWI wameiomba Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kutoa
msukumo kwa Serikali kwa baadhi ya taasisi kuendelea kuunga mkono juhudi za
mapambano ya maradhi ya UKIMWI kwani hakuna taasisi ambayo haijaguswa na
changamoto ya maradhi ya UKIMWI
Katibu Mkuu
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais alieongozana na Mkurugenzi Mtendaji Tume ya
UKUMWI na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa ZAYEDESA Mama Shadya Karume kisha
kutembelea kituo rafiki wa vijana na huduma za afya kilichopo Miembeni pamoja
na kutembela Kituo cha Programu ya shirikishi ya UKIMWI, homa ya ini, kifua
kikuu na ukoma.
Aidha Dkt
Shajak amezishukuru taasisi zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya UKIMWI na
kuahidi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia ZAC itaendelea kushirikiana
na kufanya kazi kwa pamoja na wadau wote wa mapambano ya UKIMWI ili lengo
lililowekwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar liweze kufikiwa
Lengo la
ziara hio ni kuona yanayoendelea kwenye vituo hivyo, changamoto wanazokabiliana
nazo na namna ya kuzitatua ikiwa ZAC
ndio mratibu wa masuala ya UKIMWI ili kujenga ufanisi katika kutoa huduma bora
dhidi ya mapambano ya UKIMWI
No comments:
Post a Comment