Habari za Punde

IGP Sirro Amekutana na IGP wa Congo na Kuahidi Kushirikiana Kuimarisha Hali ya Usalama.

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa, shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika (EAPCCO) litaendelea kuimarisha hali ya usalama kwenye nchi za shirikisho hilo kwa kufanya operesheni za pamoja na kuhakikisha wanadhibiti uhalifu unaovuka mipaka na kwa kubadilishana taarifa za uhalifu na wahalifu.

IGP Sirro amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati alipokutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi wa nchi ya DRC Congo, IGP Dieudonne Bahigwa ambaye amefanya ziara ya kikazi hapa nchini ikiwa ni siku chache kabla ya kupokea kijiti cha Uwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika lenye jumla ya nchi 14 wananchama wa shirikisho hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.