Habari za Punde

Jukwaa la Taifa la Wanawake Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Lazinduliwa.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu na Bunge Bw. Kaspar Mmuya akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Taifa la Wanawake wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania uliofanyika tarehe 28 Novemba, 2021 Hoteli Jijini Mbeya ikiwa ni kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani Desemba Mosi, yakiwa na kauli mbiu ya “Kuzingatia Usawa, Kutokomeza Ukimwi, Kutokomeza magonjwa ya mlipuko”.

NA.MWANDISHI WETU

Baraza la  Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania ( NACOPHA) limezindua Jukwaa la  Taifa la Wanawake wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania hii leo (28 Novemba, 2021), ambapo litawawezesha wanawake kupaza sauti zao kwenye sehemu husika na kuweza kusikika kwa haraka na sauti zao kufanyiwa kazi.

Jukwaa hilo limezinduliwa jijini Mbeya na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu na Bunge Bw. Kaspar Mmuya ikiwa ni kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani Desemba Mosi, yakiwa na kauli mbiu ya “Kuzingatia Usawa, Kutokomeza Ukimwi, Kutokomeza magonjwa ya mlipuko”.

Akihutubia wakati wa uzinduzi huo alisema, baraza hilo limekuja wakati sahihi kwa kuzingatia malengo yake katika kuhakikisha kunakuwa na sauti moja katika masuala yanayowahusu na kuathiri ustawi wao.

“Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU limekuwa chachu ya maendeleo na mabadiliko ya kisera, miongozo, sheria na utekelezaji wa afua mbalimbali za UKIMWI nchini, hongereni kwa kazi mnayoifanya”.

Naibu alieleza Serikali itaendelea kuunga mkono jitihada hizo ili kuhakikisha malengo yake yanatimia kwa viwango vinavyotarajiwa.

“Serikali ipo tayari na itaendelea kushirikiana na Baraza la Watu wanaoishi na VVU  pamoja na Jukwaa la Taifa la Wanawake wanaoishi na VVU nchini ili kuleta ufanisi katika mwitikio wa UKIMWI.”alisema Mmuya.

Akieleza historia ya uanzishwaji wa jukwaa hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa NACOPHA, Deogratius Rutatwa alibainisha malengo yake ikiwemo kuleta utetezi wa wanawake WAVIU ili kuweza kupata haki zao za msingi, ushirikishwaji katika tafiti mbalimbali zinazofanyika nchini hasa kuhusu njia za kupunguza maambukizi na kupata taarifa zinazohusu kundi hili, kuwajengea wanawake uwezo, kujikubali na kujitambua katika kuwapa ujasiri.

Malengo mengine ni pamoja na kupata fursa za kushiriki kikamilifu katika shughuli za mwitikio wa UKIMWI katika ngazi mbalimbali, ushirikishwaji wa moja kwa moja katika shughuli za kiuchumi pamoja na kupata nafasi za utetezi wa kundi hili katika kuhakikisha wanapatiwa haki zao za msingi ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya nchini.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa NACOPHA Bi.Leticia Mourice alisema, uwepo wa jukwaa utasaidia kuchochea dhana ya ushirikishwaji wa wanawake WAVIU katika masuala yanayowahusu ili kujiletea maendeleo yao na kuwawezesha kutambua fursa na kushiriki kikamilifu katika masuala ya mbalimbali.

Sambamba na hilo alisema Jukwaa hilo limeundwa kufuatia marekebisho ya Katiba ya Baraza yaliyofanyika mwaka 2013, ulionekana umuhimu wa kuwa na Jukwaa la Wanawake wanaoishi na maambukizi ya VVU kama ilivyoainishwa kwenye Sura ya Sita Ibara ndogo ya 2 na ya 6, ambayo inaelezea kuwa Baraza litakuwa na wajumbe wa Bodi kutoka Jukwaa la Wanawake WAVIU na Jukwaa la Vijana WAVIU.

“Kuundwa kwa Jukwaa hili kumetoa mwanga wa kuongezeka kwa wigo mpana wa kuwashirikisha wanawake WAVIU katika masuala yanayohusu maisha yao, kwa masalahi yao na jamii kwa ujumla. Jukwaa hili litatoa nafasi muhimu ya ushirikiano miongoni mwa wanawake WAVIU kupaza sauti zao katika mtazamo chanya wa umoja na upendo,”alieleza Leticia.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge masuala ya UKIMWI Mhe. Fatma Taufiq alipongea jitihada hizo na kuahidi kutoa ushirikiano kuhakikisha mipango na mikakati yao inafikiwa na kutambulika kama ilivyokusudiwa.

Alitumia fursa hiyo kuwaasa wanawake nchini kujiamini, kujitambua na kujua nafasi zao ili kutoishi kwa matumaini bali kwa malengo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NACOPHA, Deogratius Rutatwa akiongoza hafla ya uzinduzi huo.

Mwenyekiti wa NACOPHA Bi.Leticia Mourice akieleza historia ya kuanzishwa kwa Jukwaa la Wanawake wanaoishi na VVU nchini wakati wa uzinduzi huo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya UKIMWI Mhe. Fatma Taufiq akieleza mikakati ya kamati yake katika kuunga mkono jitihada zinazofikiwa katika kuhakikisha mapambano dhidi ya UKIMWI nchini.
Mratibu wa Programu ya Udhibiti wa UKIMWI Shirika la UNWOMEN, Jacob Kayombo akitoa salamu za shirika lake wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo wakifuatilia uzinduzi huo.

Viongozi wa Jukwaa la Taifa la Wanawake wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania wakitambulishwa kwa mgeni rasmi (Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu na Bunge Bw. Kaspar Mmuya) wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo JIjini Mbeya.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu na Bunge Bw. Kaspar Mmuya akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya UKIMWI Mhe. Fatma Taufiq, kushoto ni Mwenyekiti wa NACOPHA Bi.Leticia Mourice.

NA.MWANDISHI WETU

Baraza la  Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania ( NACOPHA) limezindua Jukwaa la  Taifa la Wanawake wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania hii leo (28 Novemba, 2021), ambapo litawawezesha wanawake kupaza sauti zao kwenye sehemu husika na kuweza kusikika kwa haraka na sauti zao kufanyiwa kazi.

Jukwaa hilo limezinduliwa jijini Mbeya na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu na Bunge Bw. Kaspar Mmuya ikiwa ni kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani Desemba Mosi, yakiwa na kauli mbiu ya “Kuzingatia Usawa, Kutokomeza Ukimwi, Kutokomeza magonjwa ya mlipuko”.

Akihutubia wakati wa uzinduzi huo alisema, baraza hilo limekuja wakati sahihi kwa kuzingatia malengo yake katika kuhakikisha kunakuwa na sauti moja katika masuala yanayowahusu na kuathiri ustawi wao.

“Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU limekuwa chachu ya maendeleo na mabadiliko ya kisera, miongozo, sheria na utekelezaji wa afua mbalimbali za UKIMWI nchini, hongereni kwa kazi mnayoifanya”.

Naibu alieleza Serikali itaendelea kuunga mkono jitihada hizo ili kuhakikisha malengo yake yanatimia kwa viwango vinavyotarajiwa.

“Serikali ipo tayari na itaendelea kushirikiana na Baraza la Watu wanaoishi na VVU  pamoja na Jukwaa la Taifa la Wanawake wanaoishi na VVU nchini ili kuleta ufanisi katika mwitikio wa UKIMWI.”alisema Mmuya.

Akieleza historia ya uanzishwaji wa jukwaa hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa NACOPHA, Deogratius Rutatwa alibainisha malengo yake ikiwemo kuleta utetezi wa wanawake WAVIU ili kuweza kupata haki zao za msingi, ushirikishwaji katika tafiti mbalimbali zinazofanyika nchini hasa kuhusu njia za kupunguza maambukizi na kupata taarifa zinazohusu kundi hili, kuwajengea wanawake uwezo, kujikubali na kujitambua katika kuwapa ujasiri.

Malengo mengine ni pamoja na kupata fursa za kushiriki kikamilifu katika shughuli za mwitikio wa UKIMWI katika ngazi mbalimbali, ushirikishwaji wa moja kwa moja katika shughuli za kiuchumi pamoja na kupata nafasi za utetezi wa kundi hili katika kuhakikisha wanapatiwa haki zao za msingi ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya nchini.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa NACOPHA Bi.Leticia Mourice alisema, uwepo wa jukwaa utasaidia kuchochea dhana ya ushirikishwaji wa wanawake WAVIU katika masuala yanayowahusu ili kujiletea maendeleo yao na kuwawezesha kutambua fursa na kushiriki kikamilifu katika masuala ya mbalimbali.

Sambamba na hilo alisema Jukwaa hilo limeundwa kufuatia marekebisho ya Katiba ya Baraza yaliyofanyika mwaka 2013, ulionekana umuhimu wa kuwa na Jukwaa la Wanawake wanaoishi na maambukizi ya VVU kama ilivyoainishwa kwenye Sura ya Sita Ibara ndogo ya 2 na ya 6, ambayo inaelezea kuwa Baraza litakuwa na wajumbe wa Bodi kutoka Jukwaa la Wanawake WAVIU na Jukwaa la Vijana WAVIU.

“Kuundwa kwa Jukwaa hili kumetoa mwanga wa kuongezeka kwa wigo mpana wa kuwashirikisha wanawake WAVIU katika masuala yanayohusu maisha yao, kwa masalahi yao na jamii kwa ujumla. Jukwaa hili litatoa nafasi muhimu ya ushirikiano miongoni mwa wanawake WAVIU kupaza sauti zao katika mtazamo chanya wa umoja na upendo,”alieleza Leticia.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge masuala ya UKIMWI Mhe. Fatma Taufiq alipongea jitihada hizo na kuahidi kutoa ushirikiano kuhakikisha mipango na mikakati yao inafikiwa na kutambulika kama ilivyokusudiwa.

Alitumia fursa hiyo kuwaasa wanawake nchini kujiamini, kujitambua na kujua nafasi zao ili kutoishi kwa matumaini bali kwa malengo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.